ALIYEVALIA SARE ZA POLISI ILI KUMPA DADAKE MAJIBU YA MTIHANI AJIPATA MATATANI BAADA YA KUPIGA SALUTI KWA AFANDE ASIYE NA CHEO.

 ALIYEVALIA SARE ZA POLISI ILI KUMPA DADAKE MAJIBU YA MTIHANI AJIPATA MATATANI BAADA YA KUPIGA SALUTI KWA AFANDE ASIYE NA CHEO.


Ndugu mmoja aliyevalia kama afisa wa polisi ili kumpa dada yake majibu ya mtihani nchini India amejikuta mikononi mwa polisi.
POLISI nchini humo umesema umesema kachero huyo feki wa polisi alinaswa akiwa na majibu hayo ya mitihani Ili kumpa dadake pindi tu alipofika kituo cha mtihani.

Kulingana na ripoti, dada wa mtu aliyetajwa hapo juu alifanya mtihani wa darasa la 12 katika Shule ya Upili ya Shababu Urdu huko Pator, jimbo la Maharashtra, magharibi mwa India.

Kulingana na maelezo, Anupam Madan Khandre mwenye umri wa miaka 24 alipanga kwenda katika kituo cha mitihani kwa kujifanya afisa wa polisi bandia.

Kwa ajili hiyo, alichukua sare ya polisi na kuingia katika kituo cha mtihani akiwa amevaa, lakini mpango wake ulivunjwa wakati timu ya polisi halisi ilipofika hapo, ikiongozwa na inspekta.

Alipoiona timu hiyo, kijana huyo aliyejawa na hofu alipiga saluti,Tena kwa polisi asiye na cheo,jambo ambalo lilianza kutia shaka kwa timu ya polisi, walipompekua walikuta kitambulisho bandia cha polisi na nakala za majibu ya mtihani hiyo ambayo alikamatwa.
Nchi ya India ni moja Kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa wanafunzi wake kuingia na majibu ya mtihani (vibomu)wakiingia navyo wenyewe ama kuletewa na watu wengine wasio wanafunzi

Comments