HELABET YAMPA DILI NONO WEMA SEPETU,MWENYEWE AFUNGUKA

 HELABET YAMPA DILI NONO WEMA SEPETU,MWENYEWE AFUNGUKA


Dar-es-Salaam,Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Helabet leo imemtangaza,Mtangazaji na Msanii wa filamu nchini Wema Isack Sepetu kama balozi wa kampuni hiyo

Hafla ya kumtangaza Msanii huyo mbele ya wanahabari umefanyika hii leo Katika hotel
i ya Four Points Jijini Dar es salaam,Leo Machi 15,2024




Akizungumza katika mkutano huo,Wema amekishukuru kampuni ya Helabet kumchagua yeye Kama balozi wake ambapo pia amesema kuwa amefurahi kuwa mwanafamilia mpya kutoka kwenye namba moja ya kampuni ya kubashiri ya michezo.

"Sikuwahi kubet hata siku moja lakini baada ya kampuni ya Helabet kunifuata na kuniaproach na Mimi nimeanza kubet na hakika kubet ni mchezo unaobadilisha maisha kwa wengi"amesema 

Hata hivyo ameongeza kuwa yeye Kama Msanii huwaga hafanyi kazi  na kampuni ambayo haiko vizuri lakini kwa kuona hii kampuni ya hela bet inafanya vizuri kwa upande wa michezo mtandaoni nikaona nishirikiane nao ili tuweze kufanya kazi.

Aidha amesema kuwa kwa Sasa ni vyema watanzania wakaanza kuitumia kampuni hiyo ya mchezo wa kubashiri mtandaoni ili kujiingizia kipato.

Comments