KINONDONI YAONGOZA UGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA

 KINONDONI YAONGOZA UGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA 




Waziri wa afya,Ummy Mwalimu amesema Bado Kuna maambukizi ya vimelea vya ugonjwa wa Matende na Mabusha kwa asilimia 2 katika kata 10 pekee kwa Mkoa wa Dar es salaam ambazo zote ziko katika Wilaya ya Kinondoni.

Waziri Ummy ameyasema hayo hii leo jijini Dar Es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hali ya udhibiti wa magonjwa hayo nchini hususan Mkoa wa Dar es salaam ambapo amezitaja kata hizo kuwa ni Tandale,Kijitonyama,Mzimuni,Mwananyamala,Kigogo,Ndugumbi,Mzimuni,Magomeni,Hananasif, Kinondoni na Magomeni.

Hata hivyo Waziri Ummy amezipongeza Halmashauri za manispaa za Temeke,Kigamboni,Ilala na Ubungo kwa hatua kubwa zilizopiga katika kutokomeza magonjwa hayo kwa kudhibiti maambukizi yake.

Comments