KONGAMANO LA THAMANI YA BINTI MWENYE NDOTO LAFANYIKA DAR,MABINTI WASHAURIWA KUTOKATISHANA TAMAA.

 KONGAMANO LA THAMANI YA BINTI MWENYE NDOTO LAFANYIKA DAR,MABINTI WASHAURIWA KUTOKATISHANA TAMAA.

Mkurugenzi wa taasisi ya Voice of Eagle Tanzania Meshack Mafyeko akizungumza katika kongamano hilo 






NA THADEI PRAYGOD,DAR ES SALAAM

Kongamano la Thamani ya binti mwenye ndoto 2024 limefanyika katika ukumbi wa mikutano,Mlimani City Jijini Dar Es Salaam na kuwakutanisha mabinti mbalimbali wenye ujuzi na wadau wengine.


Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi  taasisi inayojihusishaa na utoaji wa mafunzo ya ujuzi kwa vijana na mabinti, Voice of Eagle Tanzania ambao ndiyo waratibu wa kongamano hilo,Meshak Mafyeko amesema lengo la kuandaa kutaniko hilo ni ili kutambua mchango wa mabinti katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,biashara na taaluma kwa kuwakutanisha na watu wengine Ili kuongeza thamani ya vitu wanavyovifanya na kujiendeleza zaidi ya pale walipo kupitia hamasa na shuhuda mbalimbali za mabinti na wanawake waliofanikiwa.


Amesema kuwa kupitia Thamani ya binti mwenye ndoto mabinti mengi kupitia kongamano hilo  wamepata shuhuda kutoka kwa wanawake na mabinti wengine kwa jinsi walivyopitia mpaka kupata mafanikio kupitia shughuli wanazofanya na changamoto walizopitia.


Aidha aliongeza kuwa taaisisi ya Voice of Eagle Tanzania iliamua kuja na kampeni ya binti mwenye ndoto ili kuwapa mwamko mabinti waliokata tamaa na kuona kwamba hawawezi kufanya Chochote kutambua kuwa inawezekana kuamka Tena na kufanya kile ambacho walishindwa kukifanya kwa Kukata tamaa na tayari wamewafikia mabinti zaidi ya 500 kwa kuwapa ujuzi na mafunzo mbalimbali kwa nadharia na vitendo ikiwemo ushonaji na hata kuwasaidia vitendea kazi.


"takwimu zinasema kuwa wanawake ni wengi zaidi na Kama utamwezesha mwanamke utakuwa umeiwezesha jamii na sisi baada ya kuona taasisi nyingi zimewekeza zaidi kwa wanawake tukaona tuanzishe Voice of Eagle ili kuwaonyesha mabinti waliokata tamaa kuwa inawezekana kuinuka tena na tukaanza kuwawezesha kiujuzi na kimtaji kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo hivyo jamii inatakiwa kutambua mchango wa thamani ya binti mwenye ndoto" alisema Meshack 


Aidha aliongeza kuwa kutokana na kutambua mchango wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kulitangaza Taifa taaisi hiyo inatarajia kuja na 'Binti Mwenye ndoto Royal Tour' yenye lengo la kuwaonyesha mabinti wa Tanzania vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini Kama sehemu ya utalii wa ndani ili kuwa mabalozi wazuri wa utalii hapa nchini wakiunga Mkono Jitihada za Rais DKT Samia.


Kwa upande wake balozi wa heshima wa visiwa vya Shelisheli hapa nchini Maryvonne Pool amesema ana tambua mchango wa mabinti wenye ndoto hapa nchini na atahakikisha anawasapoti kwa kila wafanyalo huku akiipongeza taasisi ya Voice of Eagle Tanzania kwa kuwekeza kwa mabinti.


Hata hivyo ameahidi kutoka cherehani mbili za umeme kwa mabinti wawili walipata mafunzo ya ujuzi kwa kupitia taaisis ya voice of Eagle Tanzania 



Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi na mwanzilishi wa taasisi ya Msichana Initiative na Shule direct Faraja Nyalandu amewataka mabinti hapa nchini kutokata tamaa na kile wanachokifanya Kama sehemu ya kujitafuta kufikia mafanikio yao na wana budi kusapotiana Kama wanawake na kuacha kukatishana tamaa.


Faraja aliongeza kuwa mabinti wengi wamekuwa wakikata tamaa mapema na kujiona hawawezi lakini Kama watatambua thamani yao kwa jamii watafanikiwa kutimiza malengo yao.


"hata Mimi mnaniona hapa Leo Kama Mkurugenzi nilianza safari yangu Kama Miss Tena baadaye nikawa Miss Tanzania na Kama mnavyojua kwenye mashindano Yale mabinti tunavyovaa lakini sikutaka Kukata au kukatishwa tamaa na yeyote na ile ndiyo ilikuwa njia yangu ya mafanikio hivyo tusiangalie tunatumia njia gani kufikia malengo yetu tupambane Kama mabinti"alisema.




Naye Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ujenzi ya Ibra Construction Bi Zauja alisema yeye alianza Kama fundi cherehani tena akiwa ni Binti mwenye elimu ya kidato Cha nne pekee lakini Sasa anamiliki zaidi ya kampuni Tano ikiwemo ya ujenzi ambayo imekuwa ikipata tenda mbalimbali kutoka serikalini ikiwemo ujenzi wa Barabara na madaraja na hakukata tamaa katika kujitafuta mpaka alipo hivi Sasa"


"Mimi hapa mnayeniona hii leo nilianza kushona nguo miaka Mingi iliyopita tena nikiwa nimemaliza kidato Cha nne tu lakini kwa sasa namiliki makampuni makubwa na nilijiongeza kielimu ambapo kwa Sasa nina Advance Diploma,hivyo mabinti tusikate tamaa kwani huwezi kuanza bila kuwa na Chochote halafu baadaye ufanikiwe inatakiwa uwe na Cha kuanzia na Mimi nilianza kama Fundi Cherehani,mshona nguo"alisema.

Comments