MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA, SEKTA YA MADINI YAKUSANYA SHILINGI TRILIONI 1.93, ni kutokana na ada mbalimbali, mirabaha, faini na penati
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemsemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
KATIKA kipindi cha kuanzia mwezi Machi 2021 hadi Februari 2024 Wizara ya Madini imefanikiwa kuiendeleza sekta kwa namna mbalimbali ikiwemo kukusanya maduhuli yatokanayo na ada mbalimbali, mirabaha, faini na penati na kufikisha kiasi cha shilingi trilioni 1.93.
Hayo yamebainishwa leo Machi 24, 2024 na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akizungumza na Wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
"Awali mwaka 2021/22 ilikuwa shilingi bilioni 591.5 lakini hadi kufikia mwaka 2023/24 imefikia shilingi bilioni 690.4," amesema Matinyi.
Aidha Matinyi amebainisha kuwa, katika kipindi cha Machi 2021 hadi Februari 2022 mauzo ya madini mbalimbali yalikuwa shilingi bilioni 157.34 lakini kufikia kipindi cha Machi 2023 hadi Februari 2024 mauzo yamefikia shilingi bilioni 476.8.
Comments