MKUU WA WILAYA YA ILALA AIPONGEZA AKIBA COMMERCIAL BANK PLC KWA KUFUTURISHA WATEJA, WAFANYAKAZI NA WADAU WA MBALI MBALI.

 MKUU WA WILAYA YA ILALA AIPONGEZA AKIBA COMMERCIAL BANK  PLC KWA KUFUTURISHA WATEJA, WAFANYAKAZI NA WADAU WA MBALI MBALI.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo akizungumza wakati Benki ya ACB ilipoandaa hafla ya kufuturisha wateja, Wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Benki hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena tarehe 25 Machi, 2024.



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameipongeza  ACB kwa kuandaa hafla ya kufuturisha wateja, Wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Benki hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena tarehe 25 Machi, 2024.

Akiongea katika hafla hiyo ambayo Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Ilala ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi, Mhe. Mpogolo amesema kwamba,

 “kitendo cha kufuturisha kilichofanywa na ACB  ni ibada  ambayo mwanadamu  aliyetunukiwa zaidi anatoa kwa wengine na atapata thawabu kwa kufanya hivyo”.

Aidha, ameipongeza ACB kwa kuwa sehemu ya ukuwaji wa uchumi wa Tanzania na kuahidi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwa karibu na taasisi za fedha hususan benki ya Akiba katika kuinua uchumi wa nchi na kuleta maendeleo katika jamii.

Comments