MWALIMU LWAITAMA ASEMA WAZEE NI HAZINA KUBWA KATIKA VYAMA,AWATAKA WAZEE ACT KUWAFUNDA VIJANA WAO.
MWALIMU LWAITAMA ASEMA WAZEE NI HAZINA KUBWA KATIKA VYAMA,AWATAKA WAZEE ACT KUWAFUNDA VIJANA WAO.
Na mwandishi wetu,Dar es salaam
Ngome ya wazee ACT-Wazalendo wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuiunganisha jamii na kuwa moja licha ya kuwepo kwa mitazamo tofauti jambo ambalo litaepusha mifarakano ndani ya chama,vyama vya siasa na jamii kwa ujumla ikiwemo kuwafunda vijana wa vyama vya upinzani kuachana na Mihemko na siasa za kushambuliana.
Wito huo umetolewa leo Machi 1/2024 na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA Prof Azaveli Lwaitama Wakati akifungua Mkutano wa pili wa Ngome ya Wazee ACT-Wazalendo,ambapo amesema wazee ndiyo washauri wakubwa ndani ya vyama vya siasa hivyo wana kazi yao kubwa ya kuwaelimisha na kuwashauri vijana kuachana na siasa za kushambuliana na kukebehi vyama vingine Jambo ambalo linaleta mipasuko miongoni mwa vyama hivyo .
Mwalimu Lwaitama amewataka wazee hao wa chama Cha ACT WAZALENDO kuwashauri vijana wawe wanatafakari kabla ya kuzungumza ili wasije kukashifiana na kutengana na vijana wa vyama vingine kwani ili chama kishikie dola ni lazima kiwe na ushirikiano na vyama vingine.
Ameongeza kuwa nadharia nyingi hutokana na mapokeo, wazee wameona mengi na wanajua vingi vinavyowafanya kuona mbali hivyo huweza kuonya mambo mabaya kabla ya kutokea.
"Kazi ya wazee katika chama na jamii ni kupunguza moto wa vijana".alisema
Aidha amesisitiza kuwa hakuna chama kimoja kitakacholeta ukombozi kunapaswa kuheshimiana kwa vyama vya upinzani ili kuweza kuweza kushika dola.
Kwa upande wake Askofu mwamakula amesema viongozi wadini wamekuwa wakionya mambo mbalimbali yanayooneka kutoenda vizuri hususani yeye amekuwa akionya mara kwa mara kwa pande zote iwe vyama vya siasa na serikali.
Amewataka wagombea watakao shinda kwenye uchaguzi huo kuwatumia washindani wake na wazee wengine kuwashauri katika utendaji wao na watambue kuwa wao sio wenye hekima zaidi bali wamepita ili kuwatumikia wengine.
Awali akizungumza katika mkutano huo mkuu wa ngome wa wazee,mwenyekiti wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Issa Ponda amesema suala la wazee kutumika na umma ni swala kubwa mno kwani wazee ni watu wakuheshimika sana katika jamii kwakuwa wana uzoefu mkubwa katika maswala mbalimbali kisisasa hivyo chama inabidi kiwatumie Kama washauri wa masuala mbalimbali ya siasa za kitaifa na kimataifa.
"Kikao cha leo kinawezekana kikaomekana kidogo lakini nikikao kikubwa zaidi naweza kusema kuwa kikao hiki ndio kikao kikuu cha chama.Wazee ndio nguzo kuu ya kufikiri ni kisima cha fikra na busara".
Aidha mkutano huo pamoja na mambo mengine unalenga kufauchaguzi wa viongozi wa Ngome hiyo.





Comments