NABII SUGUYE KUADHIMISHA MIKA 17 YA KANISA LAKE LA (WRM) APRIL 01/2024.

 NABII SUGUYE KUADHIMISHA MIKA 17 YA KANISA LAKE LA (WRM) APRIL 01/2024.

 


Na Mwandishi wetu,

Dar es salaam.

Kanisa la The World of Reconciliation Ministry (WRM) litaadhimisha miaka 17 tokea kuanzishwa kwake siku ya Tarehe 01/04/2024 Ambapo Kanisa hilo lina mengi ya kujivunia katika kusaidia jamii kiroho na kimwili.

Akizungumza na waandishi wa habari mwanzilishi wa Kanisa la WRM Nabii Nickolas Suguye Amesema Kanisa limefanya mengi ikiwemo kusaidia Wajane,wazee na watoto yatima,pia wamefanya juhudi mbalimbali katika kuboresha Miundombinu ya barabara ambapo walichagiza kufanywa maboresho ya barabara ya kivule na baadae Serikali ikawadaidia kuiweka lami.

Pia wamekuwa wakitoa misaada ya vifaa tiba katika hospital Mbalimbali ikiwemo hospital ya rufaa ya kivule.

"Tarehe hiyo ni siku kubwa mno ambapo tulimwalika na tulitarajia kuwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lakini kutokana na mwingiliano wa ratiba amemuagiza Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Ndg Jerry silaa ili kumwakilisha na kuwa mgeni rasmi siku hiyo".

Ameongeza kuwa siku hiyo ya maadhimisho kutakuwa na usafiri bure kuanzia banana kwenda kanisani,pia huduma mbalimbali ikiwemo chakula na vinjwaji vitatolewa bila gharama zozote.

Pia siku hiyo itapambwa na matukio mbalimbali ikiwemo burudani kutoka kwa wwimbaji wa nyimbo za injili,vikundi vya kwaya,huduma za maombi na maombezi.

"Mara baada ya tukio hilo muendelezo wa kuwasaidia yatima na wajane itaendelea kwani tumejijengea utamaduni huo".

"Katika maadhimisho yetu ya miaka 17 maombezi hayawezi kuepukika siku hiyo chakula ukila pale kama unashida mbalimbali ukila chakula kile moja kwa moja kinaenda kushugulika na matatizo uliyo nayo na kitaenda kuwafungua katika maisha yao" Amesema Nabii Suguye 

Aidha katika maadhimisho hayo ya miaka 17 ya WRM wamealika watu mbalimbali ikiwemo Manabii kutoka makanisa mengine,wachungaji,wanasiasa na makundi mengi Mbalimbali.


Comments