Skip to main content

SANLG KUTOA "KITITA" KWA ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA WAUZAJI WA PIKIPIKI FEKI

 

 SANLG KUTOA "KITITA" KWA ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA WAUZAJI WA PIKIPIKI FEKI


Mkurugenzi Mkuu wa Route Marketing Consultancy Anisa Nkulo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uwepo wa biashara ya pikipiki feki za SANLG nchini.

Mratibu Mkuu wa Mradi wa Kampuni hiyo, Bahari Leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya SANLG WORLD INVESTMENT LTD imesema kuwa kuna pikipiki feki zinazotumia nembo ya SANLG kinyume na kanuni na sheria za biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Route Marketing Consultancy Anisa Nkulo amesema wao ndio wamiliki halali wa nembo ya biashara ya SANLG na imesajiliwaMratibu Mkuu wa Mradi wa Kampuni hiyo, Bahari Leo BRELA.

"Tunawajulisha wafanyabiashara na watumiaji wote wa pikipiki Tanzania, kwamba kuna pikipiki feki zinazotumia nembo yetu ya SANLG kinyume na kanuni na sheria za biashara," amesema Nkulo na kuongeza,

"Sisi SANLG WORLD INVESTMENT LTD ndio wamiliki halali wa nembo yabiashara ya SANLG na imesajiliwa BRELA ,".

Hivyo Nkulo amebainisha kuwa wataendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya kampuni au mtu yeyote ambaye kwa ulaghai anatumia vibaya nembo ya biashara la SANLG nchini.

Amesema kwamba matumizi yoyote ya nembo ya SANLG ni kinyume na sheria na kusisitiza kuwa watawachukuliwa hatua watu wanaotumia nembo yao.

Ametoa wito kwa Watanzania kutoa taarifa endapo wataona mtu yeyote anauza au kutumia pikipiki feki za SANLG, na kwamba atakayetoa taarifa hizo atapatia zawadi ya shilingi 200,000 za Kitanzania.

Nkulo ametoa ufafanuzi kwa Watanzania kuzitambua pikipiki halisi za SANLG kwa kueleza kuwa pikipiki halisi za SANLG zina neno SANLG kwenye chuma cha mbele cha pikipiki na pia hutumia lebo za plastiki pekee.

Kwa upande wake Mratibu Mkuu wa Mradi wa Kampuni hiyo, Bahari Leo amesema madhara ya kadhia hiyo ni kutumia bidhaa isiyo na uhalisia hivyo amewataka Watanzania kuacha kutumia bidhaa feki kwani zinakwamisha maslahi yao katika biashara zao wanazozalisha kwa manufaa ya watumiaji.

Comments