SERIKALI KUFANYA MABORESHO YA CHUO CHA DIPLOMASIA. - HABARI-KITAIFA.
SERIKALI KUFANYA MABORESHO YA CHUO CHA DIPLOMASIA.
DAR ES SALAAM.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January Makamba Leo January 20/2024 amezindua kamati maalum itakayosimamia na kushughulikia mchakato wa mabadiliko na maboresho ya chuo Cha uhusiano wa kimataifa Diplomasia cha Salim Ahmed Salim.
Makamba amesema wajumbe wa kamati walioteuliwa wanasifa na wabobezi katika nyanja ya diplomasia za kimataifa na pia wameitumikia Taifa katika nyadhifa mbalimbali nchin
Aidha kamati hiyo yenye wajumbe saba huku mwenyekiti wake wao akiwa ni Balozi Khamis Kagasheki na makamo wake akiwa ni balozi Ramadhani Dau.wengine ni Profesa Masilina Chinoriga (mjumbe), Dk Salim Ali (mjumbe), Dk Singo (mjumbe), Ashumta Muna (mjumbe), Dk Shule (mjumbe), Dk Sanga (mjumbe)
Aidha Makamba amezitaja kazi za kamati hiyo kuwa ni pamoja na kupendekeza muundo wa kisheria wa uongozi wa kituo aina ya mafunzo na mitaala ya chuo, Kamati inatakiwa kuwa na uwezo wa kubuni fikra za aina ya uongozi wa chuo, Kupendekeza muundo wa uombaji wa ajira kwa watu mishi na wafanyakazi wa chuo pia itakuwa na kazi ya kujua ni namna Gani chuo kitaweza kuiendesha ikiweno kubuni namna ya njia za kujipatia pesa za kujiendesha chenyewe pia imepewa kazi ya kutoa maoni na ushauri kwa wizara kwa jambo lolote ambalo litakuwa na tija kwa chuo.
Waziri Makamba amekumbusha kuwa chuo cha uhusiano wa diplomasia cha salim Ahmed Salim ni moja ya chuo kikongwe barajni Afrika kilichojizolea sifa nyingi kutokana na kuzalisha viongozi wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Balozi Khamis kagasheki ameitaka kamati hiyo kufanyakazi kwa nguvu moyo, ueledi,kijituma Uzalendo kwa Taifa kwani wao ni kati ya watanzania wengi waliopata bahati ya kuitumikia kamati hiyoSambamba na hayo Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani Tanzania imepata Mafanikio makubwa ikiwemo kung'ara Kidiplomasia Duniani kote.
Makamba amesema katika kipindi cha miaka mitatu ishara inayoonyesha kuwa Tanzania imeng'ara Kidiplomasia namna takwimu zinavyoonyesha kiwango cha Uwekezaji mtaji 2020 ilikuwa dola bilion 1.03 uliongia huku mwaka 2023 mtaji uliongia kutoka kwa wawekezaji ni bilion 5.6.
Makamba amesema kuwa Jambo ambalo nchi inatafuta kuongeza ni Ushawiahi Duniani ili ipate misaada, mikopo ,wawekezaji waje ambapo miaka mitatu ya Uongozi wa Rais idadi kubwa ya wageni, mahitaji ya sauti yake , kauli yake kutafutwa katika mambo muhimu nje ya nchi akitolea mfano Rais alipokuwa Zanzibar kuna Vingozi wakubwa walitoka nje ya nchi kumfuata awashauri hii inaonyesha namna gani Rais Dkt Samia Suluhu Hassani anavyokubalika na busara zake zinavyohitajika.
"Nchi yetu imekuwa ikipata maendeleo na kutekeleza miradi yake ya kimkakati kwa kupata mikopo ya mashariti nafuu pia misaada hiii inachagizwa na ushawishi mzuri ukiongonzwa na Mwanadiplomasia mzuri Rais wetu ambapo pia kupitia yeye wageni wamekuwa wakija kutembele Tanzania huku mialiko mingi ikija hii haitokei kama kiongozi hana Ushawishi sisi sote tujivunie kuwa na Rais mwenye upekee wa aina yake " amesema Makamba.



Comments