TAISHAN MABATI YAMPA SHAVU LA UBALOZI MPOKI,MWENYEWE ASEMA MABATI NI TAISHAN

 TAISHAN MABATI YAMPA SHAVU LA UBALOZI MPOKI,MWENYEWE ASEMA MABATI NI TAISHAN

Mkurugenzi wa kampuni ya Taishan Technology Tanzania Limited, Andrew Sun (katikati)akimkabidhi mkataba mchekeshaji maarufu hapa nchini ambayo pia ni mtangazaji wa kituo Cha Redio Cha E-Fm Mpoki mkataba wa Ubalozi Kama balozi wa mabati ya Taishan kwa miaka miwili,kulia kwake ni Meneja wa masoko na mahusiano ya umma wa Kampuni hiyo Mussa Mahundi.



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM 

Kampuni ya Taishan Technology Tanzania Limited inayozalisha mabati ya Taishan leo imemtangaza Mtangazaji na mchekeshaji maarufu hapa nchini Mpoki kama balozi wa kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kampuni hiyo Andrew Sun amesema waliamua kumchagua Mpoki Kama balozi wake kutokana na hamasa kubwa aliyonayo hapa nchini.


Amesema kampuni hiyo ambayeo inazalisha mabati ya Taishan ambayo ni mabati Bora na yenye warantii hadi ya miaka 10 itaendelea kutengeneza mabati Bora huku akiwataka watanzania kutumia mabati ya Kampuni hiyo katika kuezeka.


Kwa upande wake balozi wa kampuni hiyo Trishan mabati Mpoki ameishukuru kampuni hiyo kwa kumpa fursa ya Ubalozi wa chapa yake ya mabati ya Taishan na kuongeza kuwa watashirikiana na kampuni Katika kuiotangaza bidhaa. Ya mabati ya Kampuni hiyo kwa watanzania.


Mpoki amesema kuwa Kampuni ya Taishan Technology Tanzania Limited inayozalisha mabati ya Taishan itaendelea kuhakikisha inazalisha mabati Bora huku akiongeza kuwa kwa mtu yoyote ambaye anataka kuezeka nyumba yake kwa mabati ya Taishan anaweza kumfuata (follow) katika kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo pia atapata punguzo kubwa la Bei za bidhaa za mabati ya Taishan.

"ukiangalia Sasa hivi matangazo mengi kwenye vyombo vya habari yanahusu uuzaji wa viwanja hivyo watu wengi wanaojenga nyumba zao watahitaji kuezeka na kampuni pekee ya kupata mabati Bora na imara ni Trisha mabati" alisema Mpoki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo Andrew Sun amesema waliamua kumchagua Mpoki Kama balozi wake kwani waliona ushawishi wake alionao katika mitandao ya kijamii hivyo Kama kampuni watahakikisha wanaendelea kutengeneza bidhaa Bora za mabati ili watanzania wapete fursa za kuezeka na mabati imara.


Andrew sun ameongeza kuwa kampuni hiyo ya Trisha umeamua kuwekeza Tanzania kutokana kuwepo Kwa fursa nyingi za uwekezaji.

Naye Meneja wa masoko na mahusiano ya umma wa Kampuni ya Taishan Technology Tanzania Limited Mussa Mahundi amesema wameamua kuwekeza katika sekta ya ujenzi ambayo imekuwa ikichangia katika sekta ya ujenzi hapa nchini na kuongeza kuwa watashirikiana na serikali ili kuhakikisha watanzania wanapata bidhaa Bora za mabati.

Amesema kuwa Kampuni ya Taishan Technology Tanzania Limited inayozalisha mabati ya Taishan Ina Ofisi (viwanda)kanda zote hapa nchini hivyo watanzania watarajie kupata bidhaa Bora za mabati kote nchini.

Comments