TRC YAJIVUNIA KUFIKIA KIWANGO CHA JUU KUELEKEA KUKAMILISHA MRADI WA SGR MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA

 

TRC YAJIVUNIA KUFIKIA KIWANGO CHA JUU KUELEKEA KUKAMILISHA MRADI WA SGR MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA




Na Mwandishi wetu,Dar Es Salaam 

Shirika la Reli nchini TRC limebainisha Ujenzi wa Miundo mbinu ya Reli unaotarajia kufikia takribani trillion 23.3 ikiwa  shilingi tillion 10 zimeshalipwa kutekeleza Mradi huo wa kimkakati ili kuhakikisha watanzania wanaaza kutumia reli ya SGR mapema.



Hayo yamesemwa jijini Dar Es salaam na Mkurugenzi wa shirika Hilo,Masanja Kadogosa alipokuwa akizungumza Katika Mkutano wa wahariri na Waandiahi wa Habari wa vyombo vya habari Machi 25 ,2024 ambapo amesema  zaidi ya Asilimia 70 ya Bajeti ya serikali imewekezwa katika ujenzi wa  Reli ya Umeme (SGR) ambapo ujenzi huo  itapunguza kero ya mizigo Bandarini.


Kadogosa amesema  Wajerumani walikuwa na wazo la kujenga Reli ya (SGR)miaka mingi iliyopita lakini leo hii Rais wa Jamuhuri wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ameweza  kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki.



Aidha amesema  ujenzi wa Reli ya SGR kutoka Dar hadi Makutopola tayari Umeshafikia Asilimia 97 ambapo kwa Mwaka fedha 2024/25 wanatarajia kuanza  Ujenzi wa SGR katika Mikoa ya Tanga ,Moshi na Arusha.



Hata hivyo Shirika la Reli (TRC), limepokea maombi kutoka kampuni za uendeshaji na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika uendeshaji wa reli.


Amesema serikali imefanya maboresho ya Sheria ya Reli Na. 10 ya mwaka 2017, ikiwezesha sekta binafsi kushiriki katika utoaji huduma za usafirishaji kupitia miundombinu ya reli, hatua inayolenga kuchochea ushindani, ufanisi na ubunifu katika sekta hiyo.



Amesema jitihada za serikali katika kuwekeza sekta ya reli zimejikita kuboresha miundombinu ya reli iliyopo, ujenzi wa reli mpya ya kiwango cha Standard Gauge, na ununuzi wa vitendea kazi kama injini na mabehewa.



"Tunategemea Machi mwaka huu kupokea vichwa vya treni vilivyochongoka jitihada hiyo.inatokana na fedha zilizotolewa kusaidia mradi wa SGR uanze kazi mara moja iwezekanavyo ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi" amebainisha Kadogosa



Kadogosa amesema pia tayari seriki imeshaingia mkataba na Benki ya Dunia wa ujenzi wa Reli ya (SGR ) Tabora hadi Isiaka huku Mradi wa Dar es salaam hadi Makutupora tayari ukiwa umefik asilimia 97 na Majaribio ya Treni ya Umeme ikiwa imefanya ziara yake ya majaribio



Aidha katika hatua nyingine TRC imezindua Jariida linaloelezea Matukio miaka mitatu ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan toleo namba 35 Januari hadi Desema 2023 hivyo haliuzwi anayehitaji kusoma linapatikana mtandaoni na ofisini TRC

Comments