ZARI NA 'SOFTCARE DIAPERS' KUTOA MSAADA HOSPITALI YA MUHIMBILI KESHO.
ZARI NA 'SOFTCARE DIAPERS' KUTOA MSAADA HOSPITALI YA MUHIMBILI KESHO.
Na Mwandishi wetu,Dar Es Salaam
Mfanyabiashara maarufu na mwanasosholisiti Zarinah Hassan maarufu Kama Zari the boss lady kesho Ijumaa March 22,2023 kwa kushirikiana na kampuni ya Doweicare Technology Limited inayozalisha na kusambaza bidhaa za Softcare ikiwemo taulo za kike na diapers za watoto wanatarajia kutoa msaada kwa Akina mama waliojifungua.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ambao ulioenda sambamba na Mwanamama huyo kusaini mkataba wa kuitumikia Softcare kama balozi kwa kipindi Cha miaka MITATU amesema kuwa watagawa msaada huo kwa Akina mama waliojifungua na ambao hawawezi kukidhi gharama za kununua za diapers kwa ajili ya watoto wao wachanga.
Zari amesema yey na Kampuni hiyo kwa kushirikiana naye Kama balozi wake watatoa msaada huo katika hospitali ya Taifa-Muhimbili ambao utakuwa na thamani ya shilingi za kitanzania Milioni 30.
"Ndugu waandishi wa habari Mimi Kama balozi wa bidhaa za Softcare diapers na pedi ninayo furaha kusaini mkataba na kampuni hii kwa Mara nyingine tena Kama balozi na kesho tutakwenda hospitali ya Muhimbili kuwaona Akina mama waliojifungua na kuwapa msaada wa diapers kwa ajili ya watoto wao wachanga waliojifungua" amesema Zari.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Doweicare Technology Limited,VICTOR Zhang amewaambia waandishi wa habari kuwa kampuni hiyo umeamua kuja na msaada huo Kama sehemu ya kuridsha kwa jamii kwani kampuni hiyo ndiyo kampuni pekee iliyosambaza bidhaa zake Tanzania nzima na ambazo huuzwa kwa bei nafuu,Jambo lililopelekea watanzania wengi kutumia bidhaa za Softcare.
Zhang amesema kuwa Kampuni hiyo inayo furaha kuendelea kushirikiana na Zari tangu miaka sita iliyopita mpaka Sasa kama balozi wake na ameleta mabadiliko makubwa ndani ya kampuni hiyo kwa kuikuza chapa 'brand' ya Softcare.
Aidha ameongeza kuwa kampuni hiyo Mara baada ya kumwongezea mkataba Zari pia imeaona ije na kampuni yake ya kuwasaidia akina mama waliojifungua ambapo kesho Ijumaa watagawa 'diapers' zaidi ya pisi 83,000 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo mgeni rasmi katika shughuli hiyo anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Albert CHALAMILA.



Comments