ACT YAICHAMBUA RIPOTI YA CAG,YATAKA WABADHIRIFU WAADHIBIWE.

 ACT YAICHAMBUA RIPOTI YA CAG,YATAKA WABADHIRIFU WAADHIBIWE.

Wa pili kutoka kulia ni Kiongozi wa ACT Wazalendo, Ndugu @dorothysemu 
Wa kwanza kulia ni Waziri Mkuu Kivuli, Ndugu Isihaka mchinjita Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Kiongozi wa actbarazakivuli idrisa_kweweta Wa kwanza kushoto ni, Waziri Kivuli wa Fedha, kizamayeye




NA MWANDISHI WETU DAR ES SALAAM 

Chama Cha ACT Wazalendo kimeichambua ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka 2022/23 ambapo imeshauri mambo mbalimbali kufanyika baada ya ripoti hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Bi Kiza Mayeye Waziri kivuli wa Baraza la mawaziri vivuli la chama Cha ACT Wazalendo anayeshughulikia fedha,uwekezaji na mifuko ya hifadhi za jamii amesema kupitia ripoti ya CAG imeonyesha deni la Taifa linavyokuwa kwa Ongezeko wa asilimia 15 linaleta taswira mbaya.


Amesema Kasi ya ukuaji wa deni Hilo siyo nzuri kwa Taifa kwani litadidimiza uchumi wa nchi kwani kwa Sasa deni la Taifa limekuwa na kufikia zaidi ya asilimia 82.35 Hali ambayo italeta athari kwani fedha zinazokusanywa sasa zitakuwa zikilipa madeni ya serikali.

Kuhusu ucheleweshaji wa malipo ya mifuko ya hifadhi za kijamii kwani imeikopesha serikali fedha ambazo hazijailipa mifuko hiyo Jambo linalopelelea mifuko hiyo kushindwa kuwalipa kwa wakati mafao yao watanzania waliostaafu,kuacha au kuachishwa Kazi.

Amesema pia suala la mifuko ya hifadhi ya kijamii kushindwa kukusanya michango ya wafanyakazi inayokatwa kila mwezi kwenye mishahara yao Hali inayochangia wastaafu kutopata mafao yao.

"Kuna taasisi binafsi na za serikali ambazo watumishi wake wanafanya Kazi zao kwa bidii,na hizo taasisi binafsi na za umma hazipeleki michango ya watumishi hao katika mifuko ya hifadhi za jamii NSSF na PSSSF hivyo serikali isimamie hili Jambo ipasavyo ili wastaafu wapate stahiki zao"alisema Mayeye 

ACT Imesema baada ya ripoti ya CAG kuonyesha fedha nyingi zikipotea kwa ubadhirifa,Waliohusika katika ubadhirifu huo  kuchukuliwa hatua Kali bila kujali nyadhifa zao kwani wametumia vibaya fedha za watanzania.

Aidha chama hicho kimelitaka Bunge liisimamie vyema serikali katika utekelezaji wake wa majukumu na kizuia ubadhirifu wa Fedha za umma kwani KAZI yake kubwa ni kusimamia serikali.

Waziri wa Fedha ahakikishe fedha zote za serikali ambazo ni Mali ya umma wa Tanzania zinapitia hazina kabla ya kuzipeleka kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ili kusaidia kujua fedha hizo zimetumikaje.

Kwa upande wake Waziri mkuu kivuli wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita amesema suala la usimamizi mbovu wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Mwendokasi CAG ameonyesha kuwa wakala wa mabasi yaendayo haraka ameshindwa kuanza mradi wa awamu ya pili wa mabasi hayo licha ya miundombinu ya Barabara yake kukamilika na mradi ni Kama umetekelezwa licha ya kutumia fedha nyingi.

Mchinjita amesema ripoti ya CAG Inaonyesha kuwa mabasi zaidi ya 132 ambayo yameharibika na kutelekezwa ambapo bilioni 3 zimetumika kununua mifumo ya Tehama ya ukusanyaji nauli na kadi za kielektroniki wakati kwa mujibu wa Temesa mabasi hayo yote yangefanyiwa matengenezo kwa shilingi bilioni 1 huku Dar ikisema umeshindwa kuendesha biashara ya mabasi hayo.

Hivyo kupitia hayo ACT imeshauri kufutwa kwa bodi ya wakurugenzi ya Dart kufuatia kasoro hizo na Mkurugenzi wa mashtaka DPP,awachukulie hatua Wote walioshiriki katika ubadhirifu wa Fedha za Dart zilizopotea.

Kiongozi Mkuu wa chama hicho Bi Dorothy Semu amesema kuwa udhaifu wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF ulioonyeshwa na ripoti ya CAG ambapo mpaka kufikia June 2023 mfuko huo Ulikuwa unaidai serikali na mashirikia yasiyo ya kiserikali kiasi Cha bilioni 

Menejmenti ya NHIF isimamie na kuhakikisha madeni yote ya yanakusanywa na ihakikishe haitoi huduma kwa wasiochangia mfuko huo.

Kuhusu ATCL ACT imeshauri serikali kulimilikisha shirika Hilo ndege zote kwani kwa Sasa inazikodisha kutoka TG hivyo wapewe ndege hizo ili kulifanya kuwa na dira ya uendeshaji wa shirika.

Comments