Skip to main content

JUMUIYA ZA KIRAIA ZATAKIWA KUFUATA TARATIBU NA SHERIA

 

JUMUIYA ZA KIRAIA ZATAKIWA KUFUATA TARATIBU NA SHERIA


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amezitaka Jumuiya za kiraia zinazoendesha shughuli mbalimbali nchini zikiwemo za kidini, kitamadumi na nyinginezo zimetakiwa kufuata taratibu na sheria ili kulinasua taifa katika nchi zinazohitaji ufuatiliaji wa karibu Enhanced Monitoring (Grey List). 

Masauni amebainisha hayo Leo Machi 26, 2024 jijini Dar es Salama Hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usajili wa Jumuiya za kiraia nchini. 

"Kutokana na kuwepo changamoto ya baadhi jumuiya za kiraia kuripotiwa kutumika kufanikisha kutenda makosa ya jinai ikiwemo utakatishaji fedha, ufadhili wa shughuli za kigaidi, usafirishaji haramu wa binadamu na biashara haramu ya siraha nchi imeingizwa kwenye Grey List" amesema.

Ameongeza kuwa licha ya taifa kuingizwa katika kundi hilo, pia wadau wa maendeleo wamepewa tahadhari hiyo kushindwa kusimamia jumuiya hizo jambo ambalo linahitaji uwepo kwa ushirikiano wa pamoja kudhibiti hilo.

Pia katika uzinduzi huo, amewataka Makatibu Tawala , viongozi Kamati za Usalama, Watendaji Kata kuhakikisha kufuatilia jumuiya hizo ili kudhibiti ambazo zinakwenda kinyume na Sheria na taratibu za nchi.

Pia amewatoa wito kwa jumuiya zinazohitaji kusajiliwa au kupewa msaada wa aina yoyote zipewe huduma hiyo haraka bila kwenda kushughulikia mahitaji yao jijini dodoma.

Pia Katibu MKuu wa Wizara hiyo, Ally Gugu amesema watashirikiana kuhakikisha jumuiya hizo zinafuata Sheria na taratibu , a nchi ili kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Aliongeza kuwa uzinduzi wa kampeni ya usajili wa jumuiya hizo utasaidia kukua takwimu sahihi ya jumuiya zilizopo na namna kizisimamia ipasavyo.

Comments