NGOME YA WAZEE ACT WÀZALENDO YAUNGANA NA MCHINJITA KUITAKA TUME YA UCHAGUZI KUKAA KANDO ILI KUPISHA TUME MPYA.

 NGOME YA WAZEE ACT WÀZALENDO YAUNGANA NA MCHINJITA KUITAKA TUME YA UCHAGUZI KUKAA KANDO ILI KUPISHA TUME MPYA.






NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM


Siku Chache baada ya Makamo Mwenyekiti wa chama Cha ACT Wazalendo bara, Isihaka Mchinjita kutoa tamko la Chama ambalo liitaka tume ya Uchaguzi ya Sasa ijiuzulu ili kupisha tume mpya huru ya Uchaguzi,Baraza la wazee la chama hicho Limesema linaunga Mkono tamko hilo.


Akizungumza na waandishi wa habari Leo April 4,2024 Mwenyekiti wa ngome ya Wazee Taifa,wa chama hicho Bw  Yasini Mohammed amesema ni vyema kwa tume ya Uchaguzi iliyopo kwa Sasa ikajiuzulu na kuipisha tume mpya ili kuendana na falsafa ya Rais DKT Samia Suluhu Hassan ya 4R.


Amesema kutokana na dosari kadhaa zilizoonekana katika uchaguzi mdogo wa marudio katika kata mbalimbali nchini umetoa taswira kuwa Sasa ni vyema kwa tume hiyo kujiweka pembeni kwani RAIS alishasaini muswada wa Sheria ya vyama vya siasa na tume huru ya Uchaguzi uliopitishwa na bunge na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali.


"Uzoefu wa chaguzi za marudio ambazo ACT Wazalendo tumeshiriki unaonyesha kuwa Tume ya Uchaguzi iliyopo inabariki wizi wa kura kwa kushirikiana na baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama na kwa vile Sheria mpya ya tume ya Uchaguzi imeweka masharti ya kupatikana kwa tume mpya kupatikana kwa utaratibu wa ushindani, kupitia kamati ya usaili sisi Kama wazee tunatoa Rai kwa tume kujiuzulu kupisha uteuzi wa tume mpya" alisema 


Hata hivyo mwenyekiti huyo wa ngome ya Wazee Taifa, ACT Wazalendo ameongeza kuwa ni Wazi kuwa tume ya Sasa inabidi kujiweka pembeni ili kupisha Rais kuteua tume mpya ya Uchaguzi ambayo imekuwa ni kilio Cha siku nyingi hata kwa  vyama vingine vya upinzani hapa nchini.


"Tume iliyopo Sasa izingatie Rai ya chama Cha Cha ACT Wazalendo ya kuitaka ijiuzulu kwani tayari muda wake umeshapita,hivyo wapishe tume mpya ambayo itaamuliwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan"aliongeza Bw Yasini Mohammed.

Comments