PARI MATCH YAMTANGAZA ZAYLISSA KAMA BALOZI WAKE,YAJA NA KAMPENI YA TWENZETU DUBAI.

 PARI MATCH YAMTANGAZA ZAYLISSA KAMA BALOZI WAKE,YAJA NA KAMPENI YA TWENZETU DUBAI.




NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM


Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Pari Match imemtangaza Mke wa Msemaji wa zamani wa Klabu ya Yanga,Zaylissa kuwa balozi mpya wa Kampuni hiyo.

Akitangaza mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar Es salaam meneja masoko wa Kampuni hiyo Levis Paul amesema waliamua kumchagua Zaylisa kama balozi wao kwa kuona ushawishi wake kwa jamii.

"Leo tunapenda kumtangaza Zaylisa kama balozi wetu na tumeingia naye mkataba kwani tuliona kwa ushawishi alionao asije kuchukuliwa na makampuni mengine,Hivyo kuanzia Leo ni balozi wetu" alisema Levis

Kwa upande wake Bi Zaylisa ameishukuru kampuni ya PARIMATCH kwa kumuamini na kuahidi kuitangaza vyema kampuni hiyo.

Katika hatua nyingine kampuni hiyo imetangaza kampeni yake ya 'Twenzetu Dubai' yenye lengo la kuwawezesha wateia wake wanaobashiri kupitia kampuni hiyo kwenda nchini Duba.

Twenzetu Dubai na PARIMATCH itadumu kwa kipindi Cha wiki 8 ambao kila wiki Mshindi mmoja atapelekwa nchini Dubai kwa siku nne ili kula Bata na kufurahia maisha.

Kampeni hiyo itawapeleka wateja wake 8 Dubai yaani mmoja kila wiki kwa watakaocheza Aviator kila Alhamis Mshindi atatangazwa.

Hata Hivyo kampuni hiyo imeeleza kuwa hata kwa wale wasio wateja wa PariMatch wajiunge na kampuni hiyo kwani watapata bonus ya Shilingi elfu 5 pale tu watakapojiunga na PariMatch kwa kuscan QR Code ambazo wataziona kwenye mabasi ya Mwendokasi na mabango mbalimbali kote nchini na kisha kucheza Aviator.

Kwa upande wake balozi wa kampuni hiyo Haji Manara amewataka watanzania kutumia fursa hiyo ili kwenda kwenye nchini Dubai na kushuhudia mazuri ya nchi hiyo ikiwemo uwanja wa ndege mkubwa na wa kisasa ambao umefunguliwa hivi karibuni ambapo safari yao italipiwa kila kitu.

"Asikwambie mtu kwenda Dubai ni Raha Sana jamani yaani ukifika tu Dubai utaona uzuri wake unaosimuliwa na hata nyie waandishi wa habari mnaweza kucheza kupitia PARIMATCH"alisema Manara

Comments