TAKUKURU KINONDONI INAENDELEA KUTOA ELIMU YA RUSHWA NA MADAWA YA KULEVYA.

 TAKUKURU KINONDONI INAENDELEA KUTOA ELIMU YA RUSHWA NA MADAWA YA KULEVYA.




Dar es salaam.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kinondoni inaendelea kutoa elimu ya rushwa na dawa za kulevya kwa vijana walioko mashuleni kupitia Vipindi vya Tv redio na Magazeti, warsha mbambali ili watambue madhara ya rushwa na dawa za kulevya na kuchukua hafua kwa maslahi ya Taifa.


Hayo yameyaelezwa na Naibu Mkuu Takukuru Mkoa wa Kinondoni Elizabeth Mokiwa mara baada ya kukutana Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Kwa lengo la kutoa Taarifa ya Utendaji kazi wao katika kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi ,2024 wamefanikiwa kupokea jumla ya malalamiko 84 ambapo yaliyohusu rushwa ni 40 yasiyohusu rushwa ni 44.


"Malalamiko ambayo hayakuhusu rushwa walalamikaji wengine wameshauriwa na mjadala kufungwa huku wengine wameelekezwa sehemu sahihi ya kupeleka malalamiko yao yanayohusu rushwa majalada yanaendelea kushughulikiwa katika hatua mbalimbali", amesema Mokiwa.


Mokiwa amesema mchanganuo wa malalamiko yaliowafikia asasi binafsi 35 ,TAMISEMI/ Manispaa19, Mahakama 6 Polisi 7, Benki 5, Elimu 3, Wizara ya Ardhi 2, TLB 1,Dini 1, JKT 1, NIDA 1, TRA 2, DAWASA 1 pia katika kipindi husika mashauri mawili 2 yametolewa maamuzi na Jamuhuri imeshinda na tumefungua mashauri mapya matatu 3 huku mashauri 19 yanaendelea mahakamani “amesema Elizabeth.


"Tutaendelea kutoa elimu ya rushwa na dawa za kulevya kwa vijana walioko mashuleni kupitia Vipindi vya Tv redio na Magazeti pia warsha mbambali ili watambue madhara ya rushwa na dawa za kulevya na kuchukua hafua kwa maslahi ya Taifa”amesema Mokiwa .


Wakati huo huo amewataka Wananchi wa Kinondoni waendelee kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na wanapopata taarifa zozote za rushwa watoe taarifa kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi kwenye namba ya dharura 113 ambayo ni bure.


Ikumbukwe kuwa TAKUKURU Kinondoni inaendelea kufuatia miradi 6 yenye thamani ya shilingi Bilion sitini na moja mia tisa na kumi laki saba na arobaini na sita elfu a miambili themanini na nne (61,910,746,284,.42) na wamebaini mapungufu machache ambayo wahusika wameshauriwa kurekebisha hayo na wanaendelea kufuatia hadi miradi itakapokamilika. 

Comments