Skip to main content

ASANTE MAMA:WASANII BONGO MOVIE WATOA YA MOYONI ,KAULI YA RAIS DKT. SAMIA KUHUSU WAO

 

ASANTE MAMA:WASANII BONGO MOVIE WATOA YA MOYONI ,KAULI YA RAIS DKT. SAMIA KUHUSU WAO





NA MWANDISHI WETU

Siku chache baada ya RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktrari Samia Suluhu Hassan kutoa kauli ya kuanza kusafiri na baadhi ya wasanii kwenye ziara nje ya nchi,hatimaye wasanii wa Tasnia ya Filamu Tanzania (BONGO MOVIE) wamejumuika kwa pamoja Kumshukuru.

 Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kauli yake ya kuanza kuwajumuisha Wasanii mbalimbali kwenye ziara zake rasmi nje ya mipaka ya Tanzania kwa lengo la kujifunza zaidi juu ya tasnia hizo imeleta hisia mbalimbali Kwa wasanii kuona SASA serikali imeanza kuthamini kazi za sanaa kwa.

Rais Samia alitoa kauli yake ya kuanza kuwajumuisha Wasanii mbalimbali kwenye iara zake rasmi nje ya mipaka ya Tanzania kwa lengo la kujifunza zaidi juu ya tasnia hizo hivi karibuni alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa Albamu ya Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Hamarmonize aliyoiita "Muziki wa Samia".

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam Muigizaji na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere amesema kuwa jambo hilo ni kubwa na wanazo sababu za kumshukuru Rais Samia.

Amesema kuwa wao kama wasanii watahakikisha wanaitumia fursa hiyo katika kujifunza, kulinda maadili na kuitangaza Tanzania vizuri kiutamaduni na kiutalii jambo ambalo litaivuta Dunia kuifahamu vyema Tanzania.

Hata hivyo Nyerere amewatahadharisha wanasiasa kuwa wasije kusema kwamba jambo analolifanya Rais Samia kuwa ni kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu kupitia kwa wasanii.

Amesema Rais Samia anafanya hivyo kama mzazi anayepaswa kuwakumbatia watoto wake wote, ambapo ameleza kitendo cha Wasanii kupelekwa nje kujifunza kitawasaidia kuwainua kiuchumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waigizaji Tanzania Chiki Mchoma amesea kuwa kitendo hicho cha Rais Samia kinakwenda kuimarisha Tasnia ya Filamu Tanzania.

Aidha wasanii hao wametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. Samia kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya kwa Tasnia nzima ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Comments