BRELA HAKIKISHENI WAMILIKI BUNIFU WANATAMBULIKA ILI KAZI ZAO ZIWANUFAISHE:MWANA FA.

 BRELA HAKIKISHENI WAMILIKI BUNIFU WANATAMBULIKA ILI KAZI ZAO ZIWANUFAISHE:MWANA FA.

Na PrayGod THADEI R ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema Serikali kwakushirikiana na Taasisi nyingine zitawezesha ukamilikaji wa sera ya miliki bunifu ambayo italeta mwanga katika kusimamia mwongozo wa hati miliki Tanzania.

Hayo amesema leo Mei 9,2024 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya miliki bunifu duniani,kwa niaba ya waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaja Naibu Waziri wa Utamaduni ,Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjumaa amesema Serikali inawahakishia Wabunifu kuwa itaondoa changamoto kwa kuweka mazingira bora ili kuimarisha kipato cha mtu mmoja mmoja nchini.

Naibu Waziri ameitaka BRELA kuhakikisha wamiliki Bunifu wanatambulika Kwa lengo la kuweza kukopeshwa na kunufaika katika kukuza biashara zao.

"Serikali inauwakika kuwa miliki bunifu zitaondoa chagamoto kwa jamii na zitaongeza ukuaji wa uchumi Kwa mtu mmoja mmoja,"alisema Naibu Waziri

Pia amesema anatambua kazi nzuri inayofanya na BRELA katika kuwaimarisha wafanyabiashara na wenye makampuni kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo.

"Tutahakikisha ifikapo mwaka 2030 kunakuwa na uwiano wa maendeleo duniani kwa kutumia miliki bunifu", amesema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa amesema masuala ya ubunifu yatasaidia kusukuma ghurudumu la maendeleo mbele hivyo wana mpango wa kuanzisha programu ya miliki bunifu katika vyuo vyote nchini lengo ni kuendeleza ubunifu hizo na kuweza kutumika kwa maslahi ya nchi.

Aidha Nyaisa amesema nchi nyingi zinaendelea duniani kwa sababu ya kueneza miliki bunifu sehemu mbalimbali ndani ya nchi zao.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya ushauri BRELA Profesa Neema Mboya amesema Maadhimisho hayo ni muhimu kuendelea kusheherekewa nchini kwani yanatoa fursa ya kukutanisha wadau mbalimbali na kuweza kujadiliana,kujifunza na kupata fursa ambazo zitasaidia kukuza bunifu za wabunifu nchini.


Comments