KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 85 YA KANISA LA TAG KUFANYIKA JIJINI DAR.
KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 85 YA KANISA LA TAG KUFANYIKA JIJINI DAR.
Na PrayGod THADEI,Dar Es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dar Es Salaam,Askofu mkuu wa Kanisa hilo Askofu, Dr Barnabas Mtokambali amesema kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Julai 14,2024 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.
Amesema kuwa Kanisa Hilo lilianzia wakati wa ukoloni mnamo mwaka 1939 huko Mkoani Mbeya na hatimaye kusambaa kote nchini.
Amesema katika kipindi Cha miaka 85 kanisa Hilo limetimiza lengo lake kuu la kusambaza na kuhubiri neno la MUNGU pamoja na kusambaza wamishionari katika mataifa mbalimbali ikiwemo Kenya,Uganda,Msumbiji,Rwanda na mataifa mengine.
Aidha ameongeza kanisa Hilo pia limeanzisha vyuo katika majimbo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni katika kuchangia uwepo wa viongozi nchini pamoja na kuanzisha miradi ya kijamii inayogusa watu kwa njia chanya ikiwemo kuanzishwa kwa shule za awali,msingi na sekondari pamoja na Vituo vya afya,vyuo vya ufundi,Vituo vya Redio pamoja na miradi ya visima vya maji pamoja na Vituo vya kuhudumia wenye uhitaji.
"tunamtukuza MUNGU kwa wema wake Leo tunatimiza miaka 85 ya kanisa na hakika dhima kuu ya maadhimisho yetu ni kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake na kutuwezesha kama kanisa kudumu ndani ya kipindi chote Cha miaka 85" alisema.
Amesema kanisa la TAG limekuwa ni sehemu ya kujenga mshikamano Kitaifa na kujenga jamii imara yenye viongozi wenye maadili na kuchangia sehemu ya maendeleo ya Taifa letu.
"Naomba pia niishukuru serikali kwa kutupa ushirikiano tangu enzi za hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere na hata Sasa serikali ya awamu ya sita kupitia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na katika kilele Cha maadhimisho yetu tunatarajia kuwapo kwa wageni zaidi ya 200 kutoka nje ya nchi" aliongeza
Hata hivyo katika hatua nyingine Askofu Dkt amesema katika maadhimisho hayo watahakikisha wanaendelea kuchangia katika maendeleo ya nchi ambapo pia watakuwa na ibada kubwa na makongamano ya vijana kutoka kote nchini,semina maalum za viongozi Wote wa juu kutoka serikalini,majeshi na watu binafsi na wale wa kidini pamoja na kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa shule mbalimbali nchini.
Pia ameongeza kuwa watajenga visima katika shule mbalimbali Jijini Dar es salaam ili kuondoka kero ya maji kwa wanafunzi na kuunga mkono Jitihada za serikali .
.png)


Comments