MAENDELEO HAYANA CHAMA-DIWANI KATA YA TANDIKA
MAENDELEO HAYANA CHAMA-DIWANI KATA YA TANDIKA
Diwani wa Kata ya Tandika iliyopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Uzahilu Athumani ameitaka Jamii kuweka mapenzi yao ya vyama pembeni pindi linapokuja Suala la Maendeleo,
Mhe Uzahilu aliyasema hayo leo tarehe 25/5/2024 alipokuwa anamalizia Ziara yake akiwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata Katika Shule ya Msingi Kilimahewa baada ya kutembelea tofauti za Msingi katika kata hiyo,
Mhe Uzahilu pia alisema Mwenyekiti wa Chama tawala Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan alitoa Maagizo
"Mwenyekiti wetu wa Chama Samia Suluhu Hassan ametuagiza Sisi Viongozi tunaomsaidia Serikalini tuwafuate Wananchi sio kukaa Ofisini kusubiri tufuatwe".
Katika kuonyesha ufanyaji kazi wake wakati wa majumuisho yake na katika kutatua changamoto za wazazi waliotaka chumba cha darasa kifanyiwe Ukarabati Diwani huyo alitaka kujua Idadi ya Vyumba vya Madarasa vyenye changamoto,akaambiwa baada ya Mahesabu ikajulikana inatakiwa mifuko hamsini ya Saruji(CEMENT) hapohapo akaanzisha harambee na yeye akatoa mifuko ishirini.
Katika kuonyesha kuwa Maendeleo hayana Chama Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani cha ACT-WAZALENDO ndugu Doto Mkumba alichangia mfuko mmoja wa Saruji kati ya Mifuko hamsini inayotakiwa kwa ajili ya kukarabati vyumba Vitano vya Madarasa.
Sanjari na hayo Diwani huyo aliwakaribisha Wananchi wote wa Kata hiyo ya Tandika Siku ya Jumamosi Tar 1/6/2024 katika mkutano wa Wazi wa Wananchi kuelezea yote yaliyofanywa na Diwani.
Comments