MANDASI STORE YAZINDUA DUKA JIPYA,UKONGA BANANA,MEYA DAR AWAPA KONGOLE

 MANDASI STORE YAZINDUA DUKA JIPYA,UKONGA BANANA,MEYA DAR AWAPA KONGOLE




Na mwandishi wetu, Dar es salaam 

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar Es Salaam,Omar Kumbilamoto ameupongeza uongozi wa kampuni ya Mandasi Store kwa kuuza simu za bei nafuu kwa watanzania kwa mikopo bila masharti magumu.


Meya Kumbilamoto ameyasema hayo Leo May 2,2024 wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka la kuuza na kukopesha simu la Mandasi Store katika eneo la Banana jijini humo ambapo amesema uwepo wa duka Hilo katika eneo la Ukonga,Banana ni fursa kwa wananchi wa maeneo hayo na maeneo ya jirani kupata simu kwa mkopo wa bei nafuu.

"uwepo wa duka hili ni fursa kwa wananchi hivyo niwasisitize kuwa duka hili linauza na kukopesha simu kwa bei nafuu sana bila masharti makali,hivyo tumieni fursa hiyo"



Mkurugenzi wa maduka hayo Abdillah Mandasi amesema kuwa tayari Kuna Ofisi zaidi ya 14 hapa nchini ambazo zinatoa huduma ya kuuza na kukopesha simu pamoja na bidhaa nyingine za kielektroniki ikiwemo kompyuta mpakato (laptop).

Akiitaja Mikoa ambayo Kuna maduka ya Mandasi Store amesema kuwa ni pamoja na Mikoa ya Arusha,Mwanza,Kigoma,Dodoma,Iringa,MorogoroNjombe,Makambako,Singida,Kahama,Katoro na Dar Es Salaam.

Amesema maduka hayo hayana masharti makubwa ili kumpatia mteja mkopo wa Simu hivyo ni masharti nafuu ambayo hayamlazimishi mteja kuwekwa fedha ya awali kama 'bond' na badala yake fedha hiyo itahesabiwa kama sehemu ya malipo ya simu hiyo.

"Maduka yetu hasa hili tulilozindua hapa Banana hayana masharti makubwa ili mtu aweze kukopeshwa simu,tunachohitaji sisi ni kitambulisho chako tuu,na kianzio na tumeshasambaa tayari Mikoa mingi hapa nchini na hii yote ni ili kuendana na Jitihada za serikali kuhakikisha kila Mtanzania anakwenda na teknolojia "alisema.

Comments