NI DKT. NDUNGULILE WHO AFRICA,RAIS SAMIA ARIDHIA AGOMBEE UKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA HILO KANDA YA AFRIKA
NI DKT. NDUNGULILE WHO AFRICA,RAIS SAMIA ARIDHIA AGOMBEE UKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA HILO KANDA YA AFRIKA.
Baadhi ya viongozi mbalimbali na mabalozi mbalimbali katika picha kwenye hafla ya kumtambulisha Dkt. Faustine Ndugulile kugombea nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (Jnicc) jijini Dar es Salaam.
NA THADEI PRAYGOD
Katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kushika hatamu katika nyanja mbalimbali ulimwenguni na barani Afrika ikiwemo sekta ya afya Leo serikali ya Tanzania imemtambulisha Dkt. Faustine Ndugulile kuwa mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ukanda wa Afrika.
Dkt Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar Es salaam atawania nafasi hiyo ambayo tayari matumaini ya kushinda kiti hicho Cha ukurugenzi mkuu WHO Afrika yameanza kuonekana baada ya kuungwa mkono na nchi mbalimbali.
Akizungumza katika hafla ya utambulisho huo Mbele ya viongozi mbalimbali wa kiserikali na wadau wa afya iliyofanyika Leo na kuhudhuriwa pia na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba, amempongeza Dkt. Ndugulile kwa kuidhinishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwania nafasi hiyo.
Waziri Makamba amesema kuwa kutambulishwa kwa Dkt. Ndungulile ni Jambo tosha kuwa Tanzania itapata mwakilishi mbobevu katika shirika Hilo hapa Afrika ambaye ana uwezo mkubwa.
"Kuidhinishwa kwa Dkt Ndugulile ni ishara ya kufungua milango ya kampeni kuelekea kuwania nafasi hiyo muhimu inayobeba maslahi ya wananchi katika masuala mazima ya afya zao"alisema na kuongeza kuwa,
Daktari Ndugulile kwa muda mrefu amekuwa ni kiongozi mchapa kazi ambaye amebobea katika masuala ya afya, akihudumu katika nafasi mbalimbali Serikalini ikwemo Waziri wa Afya, na ameafanya kazi na taasisi mbalimbali za kimataifa, hivyo ninaimani anafaa kuwa katika nafasi hiyo.
Waziri Makamba ameeleza kuwa hadi sasa wakati kampeni ya Dkt. Ndugulile ikizinduliwa ni kwamba ameshapata uungwaji mkono wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Ametumia fursa hiyo kumtakia kila laheri katika safari yake hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema ni kwa mara ya kwanza kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kutoa mwakilishi wa kugombea nafasi ya Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika.
"Mgombea wetu anauzoefu mkubwa katika masuala ya afya Duniani, hivyo hii ni nafasi sahihi kwa Dkt. Ndugulile," amesema Waziri Ummy.
Hivyo amesema kutokana na ujuzi alionao Dkt. Ndugulile katika masuala ya Afya, anaamini atapeleka uzoefu mzuri WHO hususan katika utungaji na uboreshaji wa Sera za Afya kwenye Shirika hilo.
Naye Dkt. Ndugulile ambaye nimgombea wa nafasi hiyo amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kumuamini na kumpa kibali na kumuunga mkono katika kuwania nafasi hiyo.
Amesema kuwa WHO kwa Kanda ya Afrika inasimamia nchi takribani 48, hivyo amesema kuwa miongoni mwa mambo atafanya akipata nafasi hiyo ni pamoja na kuendeleza mabadiliko katika shirika
Katika kinyang'anyiro hicho kuna nchi Tano zinazogombea huku nchi 43 za Afrika zikitarajiwa kupiga kura na kuchagua mwakilishi mmoja ambapo uchaguzi utafanyika August 2024 Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,DRC
- Get link
- X
- Other Apps







Comments