RAIS DK.MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA UFARANSA KUWEKEZA ZANZIBAR

 RAIS DK.MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA UFARANSA KUWEKEZA ZANZIBAR




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito na kuwakaribisha wafanyabiashara kutoka Ufaransa kuangalia fursa kuwekeza Zanzibar katika maeneo mbalimbali. 

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Mkutano wa majadiliano ya fursa za uwekezaji  kati ya Ufaransa na Zanzibar kutoka kwa  ujumbe wa Wafanyabiashara wa makampuni  20 ya Ufaransa katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyatty Zanzibar tarehe: 29 Mei 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema sera kuu ya uchumi wa Zanzibar ni uchumi wa buluu hivyo amewakaribisha kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta ya utalii  wa fukwe, urithi, michezo  na mikutano, sekta ya bandari, mafuta na gesi, sekta ya  bandari ikiwemo  ya makontena , uvuvi  pamoja na meli za usafirishaji wa mizigo na abiria.

Pia amebainisha fursa za  miradi ya miundombinu ikiwemo barabara, viwanja vya ndege , sekta ya nishati na maji, pamoja na kilimo cha viungo.

Rais Dk.Mwinyi amewahikikishia wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mazingira mazuri kikamilifu ya kufanya biashara na uwekezaji. 

Ujumbe huo pia uliambatana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe.Nabil Hajlaoui , Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe.Ali Mwadini na Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la MEDEF kutoka Ufaransa, Gerald Wolf.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri na sekta binafsi wameshiriki mkutano huo.

Comments