RAIS SAMIA KUTOA HOTUBA YA UFUNGUZI MKUTANO WA KIMATAIFA WA NISHATI SAFI NCHINI UFARANSA.

 RAIS SAMIA KUTOA HOTUBA YA UFUNGUZI MKUTANO WA KIMATAIFA WA NISHATI SAFI NCHINI UFARANSA.





Na PrayGod THADEI,Dar Es Salaam

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhudhuria katika Mkutano wa kimataifa wa nishati safi ya Kupikia utakaofanyika jijini Paris nchini Ufaransa.


Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dar Es Salaam Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Januari Makamba amesema mkutano huo unaotarajia kufanyika May 12-15 Rais Dkt Samia atakuwa ni mwenyekiti mweza wa mkutano ambapo pia atatoa hotuba ya Ufunguzi.

Makamba amesema mkutano huo wa kimataifa wa nishati safi ya kupikia pia utahudhuriwa na wakuu wa nchi kutoka mataifa mengine duniani,mawaziri wa sekta husika,wakuu wa taasisi,sekta binafsi pamoja na baadhi ya viongozi wakuu wa nchi wastaafu.

Ameongeza kuwa madhumuni ya mkutano huo ni pamoja na kulifanya suala la matumizi ya nishati safi ya kupikia kama agenda ya kimataifa,kutoa fursa kwa nchi washiriki kutoa ahadi za michango ya fedha sambamba na kuchukua hatua madhubuti za kisera na jinsi ya kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia yanaharakishwa.

Aidha ameongeza kuwa mkutano huo pia utahudhuriwa na watu mashuhuri ulimwenguni wakiwemo wafanyabiashara wakubwa pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteresh ambapo pia Rais Dkt Samia ataongozana na mawaziri wa sekta husika,na baadhi ya wakuu wa taasisi.

"ushiriki wa Rais Dkt Samia katika mkutano huo akiwa pia kama mwenyekiti mweza wa mkutano ni kielekezo Cha kuendelea kuibeba sera ya nishati safi ya kupikia kama Shujaa ambapo Jitihada zake zimeonekana ulimwenguni kote"alisema 

Hata hivyo katika hatua nyingine Waziri Makamba amesema Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo,Rais Dkt Samia pia atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika ikulu ya nchi hiyo yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa.

Comments