TRA:TUTASHIRIKIANA NA JUMIKITA UTOAJI, ELIMU KWA MLIPAKO
TRA:TUTASHIRIKIANA NA JUMIKITA UTOAJI, ELIMU KWA MLIPAKODI
NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesme ipo tayari kushirikiana na Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) katika kutoa elimu ya Mlipakodi kwa wananchi ili Serikali izidi kuongoza ukusanyaji Mapato na kutoa huduma bora.
Hayo yamebainishwa leo Mei 29, 2024 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa TRA Hudson Kamoga akizungumza katika semina ya Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya JUMIKITA na TRA.
"Kama TRA tunaahidi tutakuwa bega kwa bega na ninyi, na tunafanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha tunamsaidia Rais kufanikisha mipango ya Maendeleo kupitia ukusanyaji Kodi," amesema Kamoga na kuongoza,
"'Forum' hii sio ya mwisho tutaendelea kukutana, hivyo tupo tayari kwa ushirikiano na ni imaini yangu hata kwa waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii wa mikoani tutakutana nao ili nao waweze kupata uwezeshaji huu,".
Akieleza sababu ya TRA kukutana na Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii, Kamoga amesema ni kutokana na maelekezo ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata ya kutaka elimu ya Mlipakodi inawafikia Watanzania wote.
Kwamba pamoja na sababu hiyo ni kuimarisha ushirikiano na Jamii kupitia waandishi hao ikizingatiwa kuwa kupitia mitandao ya kijamii Dunia imekuwa kama Kijiji, hivyo TRA wakiitumia itakuwa rahisi elimu ya Mlipakodi kuwafikia watu wengi kwa haraka.
Kamoga ameongeza kuwa kutokana na Maendeleo ya Kidigitali, huwezi kufanikiwa bila kushirikisha waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii.
Hata hivyo wametumia fursa hiyo kuwapa elimu ya masuala mbalimbali ya nayohusu TRA ikiwemo makusanyo ya Kodi ya Kidigitali, umuhimu ya kudai risti unapofanya manunuzi, mambo ya forodha, EFD, ETS na huduma kwa mteja.
"Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii wakijua haya ni rahisi wananchi kupata taarifa sahihi za TRA, hivyo tukaona ni muhimu tukutane nanyi," amesisitiza Kamoga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUMIKITA Shabani Matwebe ameipongeza TRA kwa kuwa Taasisi ya kwanza ya Serikali kutambua na kuthamini nguvu ya mitandao ya kijamii.
"TRA ni Taasisi ya kwanza kugundua nguvu ya Digital Platform, Nyie mnajua ni jinsi gani mnapata tabu kupata taarifa ikitokea mtu amewatambua ni lazima tumpongeze, Digitali Platform haikwepeki, Mkurugenzi nikupongeze," amesema Matwebe
- Get link
- X
- Other Apps
Comments