Skip to main content

WATU 11WAFARIKI, MTIBWA SUGAR,HITILAFU YA UMEME YATAJWA

 

WATU 11WAFARIKI, MTIBWA SUGAR,HITILAFU YA UMEME YATAJWA.


Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Hitilafu ya mitambo iliyotokea ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar kinachohusika na Uzalishaji wa Sukari imetajwa kuwa chanzo cha Watu 11 kupoteza Maisha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amesema “Tukio limetokea Saa 7:30 Usiku kuamkia leo Mei 23, 2024, kulitokea hitilafu katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme. Waliofariki ni Wataalamu wa Umeme na Mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo”

Amesema kati ya waliofariki kuna Raia watatu wa kigeni kutoka Kenya, India na Brazil ambapo miili ya wote waliopoteza Maisha imehifadhiwa Hospitali ya Mtibwa Sugar huku majeruhi wawili wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala.

Comments