Skip to main content

KIJANA MDOGO AMRITHI MREMA,UWENYEKITI TLP,AAHIDI KUKIVUSHA CHAMA

 KIJANA MDOGO AMRITHI MREMA,UWENYEKITI TLP,AAHIDI KUKIVUSHA CHAMA

Mwenyekiti Mpya wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP)Mhandisi Ivan Maganza akizungumza mara baada ya kutangazwa mahindi.




NA MWANDISHI WETU,DAR

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wamemchagua Injinia Aivan Maganza kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Rashid Amir, amemtangaza Maganza kuwa mshindi baada ya kupata kura 33.huku wagombea wenzake wanne wakiangukia pua mara baada ya mwanga kishika nafasi ya pili kwa kupata kura 10 huku Stanley kura mbili na wagombea wawili wakipata kura sifuri .



Akizungumza baada ya kuchaguliwa Maganza ameahidi kukibadilisha chama hicho na kuwa cha kisasa huku akituma salamu kwa vyama vingine kwamba vijipange.

Mara tuu baada ya Kuchaguliwa nafasi ya uwenyekiti wa Chama Taifa,Maganza pia amemteua Bi Riziki Gaga kuwa Katibu Mkuu wa TLP Taifa baada ya Richard Lyimo kuasi chama ambapo pia Lyimo amevuliwa nafasi ya ukatibu mkuu na kuahidi kuunda upya sekretarieti ya chama hicho.

"Wale ambao wako TLP kwa nia ya kukivuruga chama au kukikwamisha kuanzia sasa nawatangazia waondoke…nataka nibaki na watu wanaoweza kufanya kazi,” amesema Maganza.

Makamu Mwenyekiti wa TLP Taifa Dominata Rwechungura amesema wamepata wakati mgumu sana kuandaa uchaguzi huo mara baada ya kuandika barua mara kwa mara kwa Msajili wa vyama vya siasa ambaye ni mlezi wa vyama na baadae kufanikiwa kuitisha uchaguzi ambapo ameomba wajumbe kushikamana kujenga chama hicho ambacho Hayati Mrema alikipigania kwa jasho na damu 

Awali Maganza alikuwa Mwenyekiti wa Vijana TLP Taifa,Maganza Amechukua nafasi ya aliyekua Mwenyekiti wa TLP Marehemu Agustino Lyatonga  Mrema ambaye alifariki Dunia , Agost 21, 2022,  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

 kwa upande wake katibu Mwenezi wa chama hicho Geofray Stephen Laizer amesema ni wakati wa kushikamana kwa pamoja pasipo kuangali dini wala kabila.na kuondoa makundi katika chama hicho .

Amesema baada ya kumpata mwenyekiti mpya chama kitaunda safu ya ushindi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kisha kumsimamisha mgombea urais hapo mwakani 2025 .

Uchaguzi huo umefanyika nchini ya ulinzi mkubwa wa Jeshi la Polisi wakiwa na Silaa mbali mbali kwani hapo mapema  mwaka jana uchaguzi huo uliingia dosari baada  aliyekua katibu mkuu Richard Lyimo kuahrisha uchaguzi ghafla wajumbe wakiwa ukumbini tayari kwa uchaguzi mpya wa Mwenyekiti .


Mwisho

Comments