LHRC YASHAURI BAJETI KUU YA SERIKALI KUTENGA FUNGU KUBWA MIRADI YA MAENDELEO
LHRC YASHAURI BAJETI KUU YA SERIKALI KUTENGA FUNGU KUBWA MIRADI YA MAENDELEO.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Wakili Flufence Masawe akizungumza na waandishi wa Habari. |
Na Mwandishi wetu.
Siku chache Mara baada ya bajeti kuu ya serikali Kwa mwaka 2024/25 kusomwa bungeni,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka Serikali kupunguza matumizi ya kawaida kwenye bajeti kuu na asilimia kubwa ya bajeti hiyo ijielekeze katika miradi ya maendeleo ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam wakati akitoa maoni ya LHRC kuhusu makadirio ya mapendekezo ya bajeti ya Serikali 2024/2025 kwa mtazamo wa haki za Binadamu Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Wakili Flufence Masawe ambapo amesema kwamba kwa bajeti ya sasa asilimia 70 ni matumizi ya kawaida ikiwemo kulipana mishahara,madeni,kununua magari ya kifahari,serikali kutumia miji miwili hali inayowalazimu watendaji wakuu kuishi Dar na Dodoma hivyo kutumia gharama kubwa.
Ameongeza kuwa asilimia 30 pekee ya bajeti hiyo ndiyo imetengwa kwaajili ya miradi ya maendeleo hivyo kunahaja ya Serikali kupunguza matumizi ya kawaida na kuwekeza katika miradi ya maendeleo ikiwa.
Pia Ameishauri Serikali kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali ikiwemo posho,maisha ya kifahari,magari ya gharama kubwa ambayao yanaweza kuwa na mbadala wake
Katika hatua nyingine LHRC kimetoa mapendekezo kwa Serikali kupunguza kodi ya ongezo la thamani (VAT) kwenye bidhaa zote zenye uhitaji mkubwa kwenye matumizi ya nyumbani kama vile bidhaa za chakula ili kupunguza ukali wa maisha
"Ni ukweli kwamba katika kipindi cha miaka miwili mfululizo kutokana na sababu mbalimbali za siasa ulimwenguni Gharama za maisha zimepanda ikilinganishwa na kipindi kabla ya miaka miwili".
LHRC kimeipongeza Serikali kuona umuhimu wa kugharamia bima ya afya kwa wote kwa kutafuta vyanzo vya fedha kugharamia bima hiyo hata hivyo LHRC imependekeza kuongeza uwazi juu na uwajibikaji juu ya ukasanyaji na utumiaji wa fedha hizo.
Comments