Skip to main content

GRAND GALA DANCE KUFANYIKA SUPER DOMEMASAKI WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI

 







NA THADEI PRAYGOD 

Tamasha la Grand GALA Dance 2024 linatarajiwa kufanyika AGOSTI 30 Mwaka huu ambapo waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Damas Ndumbaro anatarajia kuwa mgeni Rasmi kwenye Tamasha hilo   lotakalofamyika Super Dome Masaki

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Julai 24,2024 Mkurugenzi wa Chocolate Princes ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi Cha The Mboni Show, Mboni Masimba ambaye ndiye mwandaaji wa tamasha hilo amesema kuwa Kwa mwaka huu tamasha hilo litakuwa na burudani ya kipekee ambayo halijawahi kuonekana kwenye tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.

Masimba amesema tamasha hilo litafanyika Ogosti 30, Mwaka huu ambapo miongoni mwa wasanii watakaoburudisha ni Pacho Mwamba, Charlez Baba na wengine wengi.

Charles Baba ni mwimbaji wa bendi maarufu hapa nchini ya Twanga Pepeta amesema kupitia tamasha hilo Watanzania watarejesha Imani yao katika muziki wa dansi kwani atafanya show KUBWA ambayo hakuwahi kujifanya mwanzo

Kwa upande wake Pacho Mwamba amewaita watu wengi kujitokeza kwenye Tamasha hilo wakiwemo wanamuziki wa Tanzania ili weweze kujifunza mengi ikiwemo namna ya kuimba "live".

Comments