NI BATA MSITUNI FESTIVAL 2024,DC MAGOTI AWAITA WATANZANIA KISARAWE.

 NI BATA MSITUNI FESTIVAL 2024,DC MAGOTI AWAITA WATANZANIA KISARAWE.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Petro Magoti aliyesimama katikati akizungumza na waandishi wa Habari kweye Bwawa la Minaki lililopo ndani ya hifadhi ya msitu wa asili wa Pugu, Kazimzumbwi


Na PRAYGOD THADEI,KISARAWE

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Petro Magoti amewasihi watanzania kushiriki katika tamasha kubwa la Msituni maarufu Kama Bata "Msituni Festival"ili kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika Wilaya hiyo na kusheherekea tamaduni za Kitanzania.


DC Magoti ameyasema hayo mapema hi Leo katika Mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika Leo Julai 29,2024 katika hifadhi ya msitu wa Mazingira asilia,Pugu,Kazimzumbwi uliopo Kisarawe,Pwani ambao unasimamiwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ambao  upo takribani kilomita 5 Kutoka Gongo la Mboto,Dar Es Salaam.

DC Magoti ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kisarawe amesema tamasha Hilo kwa mwaka huu litakuwa ni la kipekee kwani watanzania watapata fursa ya kukaa katika msitu huo kwa takribani siku sita wakifurahia maisha na mandhari ya msitu huo wenye maeneo mbalimbali ya kuvutia ikiwemo,panzi mwenye rangi ya bendera ya Taifa, ushoroba na Bwawa la Minaki ambapo watapata fursa ya kuvua samaki,kutembea na mitumbwi ndani ya bwawa hilo,kuweka kempu maalum,kula na kunywa na kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya na ngoma za asili kwa siku sita mfululizo kuanzia Septemba 3 hadi 8,2024



"Tamasha hili pia litahusisha mama ntilie ambao watapika vyakula mbalimbali,mbio za pikipiki,kukimbia Msituni pia kutakuwa na samaki choma,nyama choma,ngoma za asili yaani hata wewe na mkeo mkija mkataka mchomewe mbuzi mzima,mtachomewa halafu kutakuwa na siku ya kupanda Mlima ambapo wahudhuriaji watapata fursa ya kuliona Jiji lote la Dar Es Salaam kwa takribani asilimia 75 kutokea juu ya Mlima hapa hapa Kisarawe" amesema 

Aidha ameongeza Kuwa tamasha hilo kubwa la Msituni Afrika ya Mashariki linatarajiwa kuhudhuriwa na watu takribani elfu tatu wengi wakiwa ni watalii kutoka nje ya Mipaka ya Tanzania kwa kukaa katika eneo moja na Watanzania kusheherekea utamaduni na uzuri wa asili wa Afrika  na ambapo watakaohudhuria tamasha hilo watapata Kila aina ya burudani wanayoitaka maishani kupitia utalii wa ndani sawa na dhana ya utalii hapa nchini 'Tanzania Unforgetable' yaani Tanzania isiyosahaulika.

Amesema Tamasha hilo litahusisha watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Afrika ya Kusini, Kenya,Uganda huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa shughuli hiyo ambayo itafanyika ndani ya hifadhi ya msitu wa asili,Pugu Kazimzumbwi ambapo kiingilio Cha juu kitakuwa shilingi laki moja na nusu 15,0000 kwa Watanzania kwa siku zote nne watakazokuwa ndani ya msitu huo.


Kwa upande wake Afisa Mhifadhi wa wilaya ya Kisarawe kutoka wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS)ambaye pia NI Meneja  wa hifadhi hiyo ya msitu wa asili,Pugu-Kazimzumbwi Baraka Mtemwa amewakaribisha Watanzania kutembelea hifadhi hiyo kwani watajionea vitu mbalimbali ikiwemo miti,ndege panzi mwenye rangi za bendera ya Taifa la Tanzani,Ushoroba na Bwawa la Minaki,huku akisisitiza pia huduma ya malazi kwenye mazingira ya msitu huo pia inapatika na wamejipanga vyema kuwahudumia watakaoshiriki Bata msituni Festival 

Tamasha la 'Bata Msituni Festival' ni sherehe ya kipekee ya Kiafrika inayolenga kuenzi na kukuza utalii wa mazingira na utamaduni, uzuri wa asili wa Afrika na Tanzania kwa ujumla, na watu wake kupitia utamaduni, sanaa na shughuli mbalimbali za burudani

Comments