Skip to main content

RC CHALAMILA AWATAKA WATANZANIA KUWAENZI MASHUJAA KWA KUDUMISHA AMANI NCHINI

 

RC CHALAMILA AWATAKA WATANZANIA KUWAENZI MASHUJAA KWA KUDUMISHA AMANI NCHINI



NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka Watanzania kuwaenzi mashujaa kwa kuendelea kudumisha Amani ya nchi.

RC Chalamila ametoa kauli hiyo leo Julai 25, 2024 akizungumza na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa wa Tanzania yaliyofanyika katika eneo la Mnara wa Mashujaa Mnazi mmoja Ilala Jijini Dar es Salaam.

"Wako Mashujaa walioipigania nchi hii walishatangulia mbele ya haki na wapo mashuja walio hai mfano mzuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni shujaa aliye hai kupitia kazi nzuri anayoifanya ndani ya Taifa hili ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika jamii kama vile SGR, Bwawa la Mwl Nyerere na miradi mingine mingi ya Elimu na Afya," amesema RC Chalamila.
 
RC Chalamila ameeleza kuwa siku ya Mashujaa ina umuhimu mkubwa katika historia ya Tanzania, hivyo amebainisha kuwa njia bora ya kuwaenzi mashujaa hao ni kuendelea kudumisha Amani na kuepuka viashiria vyote vya uvunjifu wa Amani
 
Kwamba, Tanzania imepitia majaribu mengi kabla ya kupatikana kwa Uhuru na amani iliyopo sasa na kueleza kuwa Amani iliyopo ni matokeo ya kazi nzuri iliiyofanywa na mashujaa waliopoteza maisha pamoja na mashujaa waliohai ambao ni viongozi waliojitoa kuilinda na kusimamia amani ya nchi , hivyo ni muhimu kila mtu kuilinda amani.
 
Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Kitaifa yamefanyika katika Mkoa  wa Dodoma ambapo Rais Dkt. Samia ameongoza maadhimisho hayo.

Comments