Skip to main content

TUZO ZA LIGAE KIGAMBONI AWARDS 2024 KUFANYIKA AGOSTI 9 WAZIRI NDUMBARO,MCHENGERWA KUNOGESHA

 

TUZO ZA LIGAE KIGAMBONI AWARDS 2024 KUFANYIKA AGOSTI 9 WAZIRI NDUMBARO,MCHENGERWA KUNOGESHA





Na Mwandishi Wetu 

WAZIRI wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye Tuzo za Ligae Kigamboni Awads 2024 zinakasofanyika Agosti 9, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Julai 26, 2024 na Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii Wilaya ya Kigamboni ambaye ndiye mratibu wa tuzo hizo Mohamed Chande akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

Chande amesema lengo la tuzo hizo ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kukuza Tasnia ya Sanaa ya Filamu Nchini.

"Tuzo hizi za Ligae Kigamboni Awards, zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka Jana na aliyekuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi Pindi chana na mwaka huu ni msimu wa pili," amesema Chande.

Amesema kuwa lengo la tuzo hizi pia ni kutambua wasanii waliofanya kazi zao vizuri ambapo tuzo 45 zitatolewa kwa kategori mbalimbali kwa wasanii, wafanyabiashara na Michezo wengine waliofanya vizuri katika nyanja mbali mbali wilayani Kigamboni

Kwa upande wake Mchekeshaji maarufu hapa nchini,Joti amewapongeza waandaaji wa tuzo hizo kwani zinakwenda kukuza thamani ya sanaa katika Wilaya ya Kigamboni ambapo pia yeye anaishi Wilayani humo.

Comments