UVCCM KUZINDUA KAMPENI MAALUM KWA VIJANA,DAR JOKATE AWAITA VIJANA KWA MKAPA.

 UVCCM KUZINDUA KAMPENI MAALUM KWA VIJANA,DAR JOKATE AWAITA VIJANA KWA MKAPA.



Na Thadei PrayGod, Dar 

Umoja wa vijana wa Chama Cha mapinduzi UVCCM-Taifa inatarajia Kuzindua Kampeni maalum itakayowakutanisha vijana kutoka kote nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam,Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Jokate Mwegelo amesema kuwa lengo la Kampeni hiyo itakayozinduliwa Julai 6,2024 katika uwanja wa Benjamini Mkapa (Lupaso) ni kujadili fursa zilizotengenezwa na zinazotengenezwa Kwa vijana hao.

Lengo lingine ni kuhamasisha vijana kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu ikiwemo kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi huo.

"Kampeni hiyo ambayo tutaizindua siku ya Jumamosi pia itakuwa ni sehemu ya kuwakumbusha vijana kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga kura zoezi litakaloanza Julai 20 mwaka huu sambamba na lile la mitaa ili kushiriki kikamilifu katika uchaguzi"amesema Jokate.

Ameongeza kuwa CCM inatambua vijana Wana nguvu kubwa ya kuibua changamoto na Usuluhishi wake hivyo chama kitaendelea kuthamini Mchango wa vijana.

"nawasihi vijana tujitokeze Kwa wingi kujiandikisha na baadaye kuamua mustakabali wa nchi yetu kupitia uchaguzi"ameongeza

Comments