JAMII YATAKIWA KUJITAFAKARI KUENDELEA ,KUWEPO KWA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO

 JAMII YATAKIWA KUJITAFAKARI KUENDELEA ,KUWEPO KWA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO



Jamii imetakiwa kukaa na kutafakari na kujiuliza ni Nini kinapelekea kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi makundi mbalimbali hasa watoto kwenye jamii hiyo.


Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya jamii,Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Hilda Malosha alipokuwa akifungua mafunzo ya udhibiti wa vitendo hivyo yaliyofanyika Jijini Dar Es salaam na Shirika la usawa wa kijinsia Tanzania (SUKITA) .

Bi Malosha amesema matoke ya uwepo wa vitendo vya ukatili NI kwa sababu watoto hujifunza ukatili kuanzia ngazi ya familia na hata wanapokuwa watu wazima huanza kuwafanyia ukatili pia wengine wakiwemo watoto hivyo jamii inapaswa kujitafakari.

"hata hivi nilivyo Mimi Kuna watu waliwekeza muda wao kwangu hivyo hivyo ni bora kwa jamii kutoa malezi Bora kwa watoto ili kutengeneza Taifa Bora baadaye"amesema

Ameongeza kuwa Kuna sababu ya jamii kurudi nyuma kwa kujiuliza pale ilipokosea ili kujirekebisha kwani Kuna madhara makubwa endapo jamii imepata malezi mabaya.

"Usipompa Mungu malezi ya mwanao,basi utampa shetani na huyo shetani atamtengeneza mwanao kuwa mtu wa hovyo kwenye jamii hivyo niwaombe wazazi na walezi wamtangulize Mwenyezi Mungu kwenye malezi ya watoto"amesisitiza Bi Malosha.



Kwa upande wake Afisa miradi wa Shirika la usawa wa kijinsia Tanzania SUKITA,Jamaica Kyando amesema baada ya kuona bado vitendo vya ukatili vipo kwenye Manispaa ya Ubungo waliamua kuja na mafunzo hayo maalum ambayo yamewakutanisha maafisa elimu kata,Polisi kata na watendaji wa kata na mitaa,pamoja na maafisa wa ustawi wa jamii.

Kyando amesema pia tayari Shirika la SUKITA limeshatoa elimu juu ya kujilinda kwa wanafunzi kuanzia wakiwa mashuleni hadi majumbani ambapo imewasaidia wanafunzi hao kuepuka kufanyiwa ukatili

Comments