WANAKISARAWE MSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA:WAZIRI JAFO

 WANAKISARAWE MSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA:WAZIRI JAFO






Na Thadei PrayGod
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe lililopo Mkoani Pwani,Selemani Jafo ambaye pia ni Waziri wa viwanda na biashara amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuchagua viongozi makini na Wazuri ambao watawaletea Maendeleo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.

Waziri Jafo aliyasema hayo Jana Agosti 31,2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige katika kuhitimisha Tamasha la Sanaa mtaa kwa mtaa lililoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa,Basata kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Waziri huyo ambaye alipanda jukwaani akiwa anasakata goma la muziki wa mtaa maarufu kama 'Singeli' akiwa ameambatana na viongozi wa Wilaya hiyo amesema ni wakati Sasa wa wana Kisarawe kuamka na kushirikiana katika kujiandikisha ili kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwakufanyika kote nchini Novemba Mwaka huu.

"Wilaya yetu imepiga hatua kubwa kimaendeleo kwa Sasa na tayari tumeshaletewa Hospitali ya Kisasa ya Wilaya,Shule ambazo zote hizi Ni jitihada za Rais DKT Samia na Sasa pia tutajenga Barabara ya Lami kwend Msanga na kufukisha umeme vijiji vyote hii Ni ishara kuwa wananchi mnatakiwa kuchagua CCM"alisema Jafo.



Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti alisema uwepo wa tamasha la Sanaa mtaa kwa mtaa Ni dhihirisho kuwa Wilaya hiyo inathamini vipaji vya vijana na itahakikisha matamasha Kama hayo yanaendelea kufanyika.

DC Magoti alisema Ni muhimu vijana wa Wilaya hiyo kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu kwa kujiandikisha na hatimaye kupiga kura ili kuwapata viongozi ambao watawavusha kwa Furaha na Amani.

Hata hivyo alitumia jukwaani hilo kuwakaribisha watanzania na wasio watanzania katika Tamasha kubwa la Bata Msituni Festival ambalo linatajiwa kukutanisha maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali kufurahi kwa pamoja na kupata burudani katika msitu wa Pugu-Kazimzumbwi kuanzia Septemba 22 mpaka 27,2024 

Tamasha la Sanaa mtaa kwa mtaa lililofanyika katika uwanja wa Chanzige liliwakutanisha kwenye jukwa moja wasanii wa Kisarawe na magwiji wa muziki hapa nchini ambapo muziki wa taarab uliongozwa na Malkia Isha Mashauzi na Mfalme Mzee Yusuph huku upande wa Singeli uliongozwa na Easy Man,Shollo Mwamba na wengine.

Comments