'Emma',Jamaa aliyeuza mradi feki wa uwanja wa ndege ambao haupo Nigeria,akawatapeli Wabrazil

 



Achana na wale jamaa wa hiyo pesa Tuma kwa namba hii, huyu hapa BABU wa Matapeli duniani.


Imagine kuuza uwanja wa ndege ambao haupo kwa dola milioni 242! Ungewezaje kufikiria kitu kama hiki? 


Hii ni hadithi ya Emmanuel Nwude,Mkurugenzi wa zamani wa mabenki nchini Nigeria na baadaye tapeli maarufu wa Nigeria aliyeuza mradi feki wa uwanja wa ndege kwa benki ya Brazil.


Soma Zaidi: 👇👇


Mwaka 1995, Emmanue alijifanya kuwa gavana wa Benki Kuu ya Nigeria na kuwasiliana na Nelson Sakaguchi, meneja wa Benki ya Noroeste kutoka Brazil.


Alimdanganya kwa ahadi ya uwekezaji katika uwanja wa ndege mpya huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria.


Emmanuel aliambia meneja wa benki kwamba serikali ya Nigeria ilikuwa inatafuta wawekezaji wa mradi wa uwanja wa ndege wenye thamani ya dola milioni 250. 


Alihakikisha kuwa huu ni mradi wa kipekee ambao ungeleta faida kubwa kwa muda mfupi.


Kwa kuongeza ushawishi, Emmanuel alimwahidi Sakaguchi kamisheni ya dola milioni 10 kama shukrani kwa kufanikisha dili. 


Sakaguchi, alifurahia uwezekano wa faida na kamisheni hiyo, akaingia kwenye 18 bila kujua kilichokuwa kikiendelea.


Mwamba Emmanuel na washirika wake waliandaa mpango mzuri kabisa.


Walijifanya maafisa wa ngazi za juu serikalini, walitoa nyaraka za uongo zilizoonekana kuwa halali.


Miamba ikapanga mikutano ya kifahari katika hoteli za kifahari ili kumshawishi zaidi Sakaguchi.


Mikutano yao ilifanyika London, ambapo walivaa na kuonekana kuwa watu mashuhuri wenye ushawishi.


Walionyesha mpango wa uwanja wa ndege, ramani za ujenzi (Engineering drawings).


Miamba ikasisitiza kuwa mradi huo unapaswa kuwa wa siri kwa miaka kadhaa kabla ya kutangazwa rasmi.


Katika hatua hii, Sakaguchi aliombwa kutuma malipo ya awali ya dola milioni 3 kama uthibitisho wa nia yake ya kuwekeza. 


Licha ya wasiwasi kidogo, alikubali na kutuma pesa hizo.


Kwa miaka mitatu, kuanzia 1995 hadi 1998, Sakaguchi aliendelea kutuma mamilioni ya dola zaidi kwa Emmanuel, akiendelea kuamini kuwa anafanya uwekezaji wa faida kubwa. 


Hakuwahi kumwambia yeyote kutoka benki yake kuhusu mchakato huo.


Hatimaye, mwaka 1998, utapeli huu mkubwa uligundulika, na Emmanuel Nwude na washirika wake walikamatwa. 


Walifanikiwa kuiba kiasi kikubwa cha dola milioni 242 kabla ya kufikishwa mahakamani.


Hata hivyo baadaye mwaka 2006 jamaa aliachiwa HURU na kisha kufungua kesi akitaka kurudishiwa baadhi ya Mali zake akidai kuwa alizipata Kabla ya uhalifu aliyoufanya

Comments