MAPITO AFRICA YAMREJESHA BINTI ALIYEPELEKWA KUWA 'HOUSEGIRL' IRAQ YAIOMBA SERIKALI KUWAFUATILIA MAWAKALA WANAOPELEKA WAFANYAKAZI NJE YA NCHI.
MAPITO AFRICA YAMREJESHA BINTI ALIYEPELEKWA KUWA 'HOUSEGIRL' IRAQ YAIOMBA SERIKALI KUWAFUATILIA MAWAKALA WANAOPELEKA WAFANYAKAZI NJE YA NCHI.
Mkurugenzi wa Mapito Africa Foundation ambaye pia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Mapito kinachoruka Global TV na Global Radio Zaliam Tabuyanjaa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
KATIKA Dunia ya leo kila mtu hutafuta shughuli ambayo itampatia kipato ili kuendesha maisha yake,ndoto ya mabinti wengi wa kitanzania hasa wanaofanya kazi za ndani hupenda kufanya kazi nje ya nchi kutokana na stori wanazosikikia kuwa nchi hizo huwalipa wafanyakazi wa ndani pesa nyingi.
Wapo waliokwenda kufanya kazi hizo za ndani na wakafanikiwawa kurudi na fedha nyingi ambazo zimewasaida kufungua biashara zao hapa nchini ama kujenga nyumba lakini wapo ambao walirudi na makovu,makovu ambayo yamewaachia machozi maishani,na simulizi zao Ni za kusikitisha.
Mapito Africa Foundation imeiomba Serikali kufuatilia usajili wa mawakala wanaosafirisha watu kufanya kazi nje ya nchi.
Ombi hilo limetolewa leo Septemba 5, 2024 na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Mapito kinachoruka Global TV na Global Radio Zaliam Tabuyanjaa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakiripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu kuteswa na kunyanyaswa kwa watu wanaoenda kufanya kazi nchi za nje hususan katika nchi za Kiarabu.
"Global TV kupitia kipindi cha Mapito tulipata pia nafasi ya kuwa miongoni mwa vyombo vya habari hivyo vilivyoripoti visa hivyo vya unyanyasaji wa mabinti mbalimbali wanaotolewa hapa nchini kwenda mataifa hayo kwa lengo la kufanya kazi na mwisho wa siku kuishia kuteswa kwa kufanyishwa kazi ambazo hazikuwa katika makubaliano," amesema Tabuyanjaa na kuongeza,
"Wamekuwa wakinyanyaswa kingono, kufanyishwa kazi ambazo hazikuwa katika mkataba na kutokuruhusiwa kurudi nyumbani endapo watahitaji kurudi,".
Kwamba kutokana na kupokea matukio hayo kwa wingi kutoka kwa wadada hao wanaopitia katika wakati huo mgumu, wamefuatilia kwa kina na kuwahoji watu hao kwa kutaka kufahamu ukweli kuhusu changamoto wanazopitia, na kubaini sababu mbalimbali zinazowafanya wao kujikuta katika wakati mgumu.
Amesema katika mahojiano hayo miongoni mwa sababu walizobaini ni kudanganywa na watu mbalimbali, kuwepo kwa mawakala feki wanaowaahidi kuwasafirisha, kuwepo kwa matangazo mengi yasiyo rasmi ya kazi za nje na kutoroshwa kwa mabinti na kupelekwa nje ya nchi.
"Kutokana na sababu hizo na nyingine nyingi ambazo zimeelezwa na wahanga tungependa kuiomba Serikali kuingilia kati Swala hili kutokana na watanzania walio wengi kuteseka wakiwa katika mataifa hayo huku sababu kuu zikiwa ni kudanganywa na watu wanaojiita mawakala ambao hawajasajiliwa na mamlaka husika na kuwasafirisha mabinti na kuwafanyisha mambo ambayo ni kinyume na haki za binadamu," ameeleza Tabuyanjaa.
Tabuyanjaa amebainisha kuwa Global TV kupitia kipindi chake cha Mpito wamefanikiwa kumsaidia Rahma Maneno aliyekuwa amekwama nchini Iraq ambaye amepitia mengi ikiwa ni pamoja na kunyanyaswa, kuteswa, kupigwa na kuzuiwa kurudi nchini mpaka nguvu za ziada zilipotumika.
Kwa upande wake Rahma akizungumzia kuhusu manyanyaso na mateso aliyopitia akiwa nchini Iraq ameishukuru Global TV na Serikali kwa kupambana na kuhakikisha anarejea nchini.
- Get link
- X
- Other Apps


Comments