Skip to main content

SASA NI KADI JANJA ZA MWENDOKASI DAR,WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA NA KUTOA MAELEKEZO HAYA KWA DART NA UDART,asema mradi huo ni wa kikmkakati

SASA NI KADI JANJA ZA MWENDOKASI DAR,WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA NA KUTOA MAELEKEZO HAYA KWA DART NA UDART,asema mradi huo ni wa kikmkakati.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza jambo wakati akizindua kadi Janja na Mageti kwa ajili ya matumizi ya abilia wakati wanatumia  Mabasi ya Yaendayo Haraka  uliyofanyika leo Septemba 2, 2024 katika Kituo cha Mabasi ya Yaendayo Haraka Kimara Mwisho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza  wakati akizindua kadi Janja na Mageti kwa ajili ya matumizi ya abiria wakati wanatumia  Mabasi ya Yaendayo Haraka  uliyofanyika leo Septemba 2, 2024 katika Kituo cha Mabasi ya Yaendayo Haraka Kimara Mwisho.

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Mabasi ya Yaendayo Haraka (DART) Dkt. Athuman Kihamia akizungumza jambo wakati wa uzindua kadi Janja na Mageti kwa ajili ya matumizi ya abiria wakati wanatumia  Mabasi ya Yaendayo Haraka  uliyofanyika leo Septemba 2, 2024 katika Kituo cha Mabasi ya Yaendayo Haraka Kimara Mwisho.



Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa Mabasi ya Yaendayo Haraka (DART) Dkt. Florens Turuka  akizungumza jambo wakati uzindua kadi Janja na Mageti kwa ajili ya matumizi ya abiria wakati wanatumia  Mabasi ya Yaendayo Haraka  uliyofanyika leo Septemba 2, 2024 katika Kituo cha Mabasi ya Yaendayo Haraka Kimara Mwisho.

NA THADEI PRAYGOD

Ili kuhakikisha huduma ya mabasi yaendayo haraka maarufu kama Mwendokasi inakuwa ya kidigitali na rahisi zaidi kwa watumiaji wa Mabasi hayo jijiJi Dar Es Salaam,WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amezindua Kadi Janja za kulipia nauli kwa ajili ya usafiri wa mabasi ya mwendokasi.

Kadi hizo Janja Sasa zitaondoa kwa kiasi fulani matumizi ya hela cash kwa abiria ambao Sasa watapaswa kuchanja tu kadi zao kweye mageti Janja na hatimaye kupanda mabasi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo leo Septemba 2, 2024 jijini Dar es Salaam Waziri Mchengerwa ameagiza Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kuhakikisha Kadi hizo zinaanza kutumika mara Moja.

Waziri Mchengerwa amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kujibu hoja za wananchi kwa kuhakikisha inatatua changamoto zao na kwamba kila mtendaji ndani ya Serikali anao wajibu wa kujibu hoja za wananchi.

"Tunazindua Rasmi huduma hii , uzinduzi huu unatokana na Maendeleo ya teknolojia katika ukataji wa Tiketi za mabasi. DART nawapongeza kwa kutekeleza dhamira na maono ya Rais Samia katika kujibu hoja za wananchi," amesema Waziri Mchengerwa na kuongeza,

"Kadi hizi zinaenda kuleta Mapinduzi makubwa katika usafiri wa Mwendokasi, Kadi hizi zina kwenda kuondoa matumizi ya karatasi,".

Hata hivyo Waziri Mchengerwa ametaka uzinduzi wa Kadi hizo uende sambamba na usafi wa mazingira katika Jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa DART Dkt. Athumani Kihamia ametaja faida zitokanazo na matumizi ya Kadi hizo kuwa ni pamoja na kuondoa usumbufu wa kupanga foleni Wakati wa ukataji Tiketi.

Kadhalika kuondoa matumizi ya karatasi, kuondoa usumbufu wa chenji wakati wa ukataji Tiketi hususan chenji ya shilingi 50, kwamba uzinduzi wa Kadi hizo unakwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo wa kuendeshea mabasi utekaofanyika hivi karibuni.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya DART Dkt. Florens Turuka amesema kuwa watahakikisha wanaendelea kufanya maboresho ya mifumo ya uendeshaji wa mradi huo na kuleta tija.

Comments