Skip to main content

WAFANYAKAZI WANAWAKE STENDI YA MAGUFULI WAPEWA MAFUNZO YA UKATILI WA KIJINSIA,UWAM WASEMA BADO KUNA CHANGAMOTO

 





NA THADEI PrayGod

UMOJA wa Wasafirishaji Abiria Mikoani (UWAM) umetoa mafunzo kuhusu mradi wa haki za Wanawake na Watoto katika Sekta ya Usafirishaji, Magufuli Bus Terminal- Awamu ya Pili.

Makundi ya Wanawake waliopatiwa mafunzo hayo ni Mawakala wa Mabasi, Mama Lishe, Wauza Vinywaji na Wabeba Mizigo.

Akizungumza leo Septemba 30, 2024 jijini Dar es Salaam Wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kibamba Beatrice Mbawala amesema kitendo cha kuwa mwanamke au mtoto kinavutia kuwa chanzo cha kupata changamoto ya utalii.

Hivyo amewataka Wanawake hao kuweka wazi changamoto zao ili Serikali iweze kuzishughulikia.

"Kama Serikali ipo tayari kupokea changamoto zao na kuweka Mpango mkakati wa kuzitatua," amesema Mbawala na kuongeza,

"Moja ya changamoto wameeleza ni kukosekana Kwa chumba cha kujihifadhi Wakati wa hedhi,".

Katika hatua nyingine Mbawala amewaomba wazazi Mikoani kutoruhusu watato wao kuja Dar es Salaam kwani wengi wanadanganywa kuwa kuwa ajira jambo ambalo linawafanya watoto waishie katika vitendo vya ukatili.

Kwamba wamekuwa wakifanya operesheni ya mara Kwa mara katika kituo cha Magufuli Bus Terminal na kiwarudisha watoto nyumbani kwao Mikoani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWAM Peter Ndengerio akizungumzia kuhusu mradi huo, amesema umelenga kushuhulokia changamoto ya vyoo na lugha za matusi ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo Wanawake na Watoto katika kituo cha Magufuli Bus Terminal.

Naye Mratibu wa Mradi huo Dahlia Majid amesema mradi huo unalenga Wanawake na Watoto waliopo eneo la Magufuli Bus Terminal.

Comments