WASANII WAJENGEWE MAKUMBUSHO:MONALISA

 WASANII WAJENGEWE MAKUMBUSHO:MONALISA 



NA MWANDISHI WETU.


Msanii Yvone Cherry maarufu kama Monalisa amesema kuna namna serikali iangalie namna ya kuwaenzi wasanii nchini kwa kuwa na makumbusho maalum ya kuonyesha kazi zao


Monalisa ameyasema hayo Leo Septemba 7,2024 katika uwanja wa Leaders Club kunakofanyika Tamasha la Faraja ya Tasnia lenye lengo la kuwaenzi wanatasnia hiyo waliofariki Dunia kwa nyakati tofauti


Monalisa ambaye Ni msanii wa filamu hapa nchini ambaye pia amekuwa akifanya kazi ya utangazaji amesema kazi za Sanaa zinabidi kuwekewa makumbusho kwani zinaweza kuwa sehemu ya utalii.



" Ni muhimu kwa Serikali kuangalia kutengeneza nyumba ya makumbusho au maktaba ya kazi za wasanii wa filamu na wanamichezo ili kutoa fursa kwa wananchiI na watalii kutembelea na kuona kazi, zilizofanywa," amesema.


Tamasha la Faraja ya Tasnia linafanyika katika uwanja wa Leaders Club Kinondoni,jijini  Dar Es Salaam leo Jumamosi Julai 7,2024

Comments