Skip to main content

ACT WAZALENDO "YALALAMIKIA" WAGOMBEA WAO KUNYIMWA FOMU KUWANIA UONGOZI SERIKALINI ZA MITAA,yamtaka Waziri Tamisemi kuwafurusha wanaokwamisha mchakato

 

ACT WAZALENDO "YALALAMIKIA" WAGOMBEA WAO KUNYIMWA FOMU KUWANIA UONGOZI SERIKALINI ZA MITAA,yamtaka Waziri Tamisemi kuwafurusha wanaokwamisha mchakato


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Bara Isihaka Mchinjita akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema wagombea wa vyama vya upinzani katika maeneo mengi nchini wamekuwa wakinyimwa fomu za kuwania uongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 31, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara Isihaka Mchinjita akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Kwamba wakati mwingine watendaji wa vijiji na Mitaa wamechukua hatua ya kiwakimbia wagombea ili wasichukue au wasirudishe fomu hizo.

Akielezea dosari katika uchukuaji fomu amesema "Maeneo mengi wanachama wa ACT wamejitokeza kuchukua fomu lakini wanapewa nakala Moja na hivyo wanatakiwa wakatoe "photocopy".

Mchinjita kudai kuwa wasimamia wamefikia hatua ya kukimbia ofisi na hawapatikani na maeneo mengine wasimamizi hudai kuwa wameshatoa fomu Kwa wagombea wa ACT huku wakijua sio kweli.

Kadhalika amedai kuwa wagombea wamekuwa wakitishiwa kwamba wasichukue fomu wala kugombea, lakini pia Kwa waliogombea wakitakiwa wajitoe.

Kwamba wagombea pia wamekuwa waidaiwa vitamburisho vya uraia huku wakitambua kua sio wote wenye vitamburisho hivyo.

Hivyo ametumia fursa hiyo kuitaka Serikali Kwa muda uliobaki kuhakikisha wagombea wote wanapatiwa fomu na kijirejesha bila vikwazo.

Comments