SIMULIZI YA KISA CHA AJABU NA CHA KUTISHA CHA 'BUS NUMBER 375' LILILOPOTEA KIMAAJABU CHINA

 KISA CHA AJABU NA CHA KUTISHA CHA 'BUS NUMBER 375' LILILOPOTEA KIMAAJABU CHINA




Basi la Mwisho la Njia 375

Hadithi hii ilitokea usiku wa giza wa Novemba 14, 1995, huko Beijing, Uchina. Mzee mmoja (wengine wanasema mwanamke mzee) alikuwa akingoja kwenye kituo cha basi usiku wa manane, huku akiwa kimya mtu mwingine pekee kwenye kituo hicho aliyefika alikuwa ni  kijana mmoja mdogo mtulivu. 

Dakika kadhaa baadaye basi la usiku wa manane 375 - basi la mwisho kwa Route 375 kutoka kituo cha mabasi cha Yuan-ming-huan - hatimaye lilifika kituoni na  wote wawili walipanda yaan yule Kikongwe na Kijana. 

Mzee huyo aliketi kwenye siti peke yake karibu na mbele ya basi huku yule kijana akiwa amekaa safu kadhaa nyuma yake.

Ndani ya basi Hakukuwa na abiria wengine pamoja nao, isipokuwa dereva na na kondakta wake wa kike.

Baada ya muda, dereva aliona vivuli viwili kando ya barabara, vikipungia basi na kwa kuwa hakuwaangalia kwa makini Alisimama, na milango ilipofunguliwa,hawakuwa watu wawili tena bali watu watatu walipanda; 

watu wawili waliokuwa wamembeba mtu mmoja katikati  wakimshikilia kwa mabega yake. Yule mtu aliyekuwa katikati alionekana amefadhaika, na kichwa chake kilikuwa kimeinama ili mtu asiweze kumuona usoni. Kulikuwa na hali mbaya na ya utulivu ndani ya basi.

Dakika chache baadaye ghafla baadaye, mzee huyo alianzisha ugomvi na kijana huyo kwa kisingizio kuwa eti kijana yule alimwibia mkoba wake , Ugomvi ulizidi, na dereva wa basi akawalazimisha wote wawili kushuka kwenye basi.

Waliposhuka na basi likaondoka mara yule mzee hakuwa na hasira tena. Alimwambia kijana huyo kwamba alikuwa ameokoa maisha yao.

"Wale abiria watatu wapya hawakuwa na miguu. Walikuwa wakielea; hawakuwa watu wanaoishi," alisema.

Baada ya hapo, walikwenda kituo cha polisi kilichokuwa karibu kuripoti kilichotokea, lakini hakuna aliyewaamini. Siku iliyofuata, kampuni ya basi ilitoa taarifa, "Jana usiku, basi la mwisho la Route 375 lilitoweka, pamoja na dereva na kondakta wake wa like

" Polisi walimfukuza mara moja mzee huyo na kijana huyo, ambao awali walidhaniwa kuwa na ugonjwa wa akili walipojaribu kutoa taarifa mapema. Wote wawili walihojiwa kwenye habari.

Siku ya tatu, polisi waligundua basi lililopotea kwenye hifadhi ya maji takriban kilomita 100 kutoka lilikokuwa likienda, Xiang-shan, au kinachojulikana kama Milima ya Kunukia. Ndani ya basi hilo kulikuwa na maiti tatu zilizoharibika vibaya sana. Siri zinazozunguka ugunduzi huu ni pamoja na:

Ukweli kwamba basi halikuwa na petroli ya kutosha kwenda mbali hivyo baada ya safari ya siku nzima.

Ukweli kwamba tanki la petroli lilijazwa na damu mbichi badala ya mafuta.

Ukweli kwamba maiti za watu watano zilipatikana,lakini kati ya maiti hizo tano miili mitatu ilikutwa ikiwa imeoza na kuharibika vibaya huku miili miwili ikiwa ni ya dereva na kondakta wake ikiwa kama imeganda tu bila kuharibika

Lakini madaktari walipatwa na shaka kuwa iweje miili mitatu kati ya mitano ya maiti zilizopatikana zilikuwa zimeoza sana kwa masaa 48 tu; hata kama ingekuwa majira ya joto, mchakato wa kuoza haungekuwa wa haraka hivi. 


Ukweli kwamba, hata baada ya polisi kupitia kamera zote za ulinzi za njia lilipopita bus hilo hawakuliona kwenye kamera na swali lililoumiza vichwa ni kuwa iweje basi lisionekane kwenye kamera za barabarani?hakikuwa kitu Cha kawaida.


Hadi leo hadithi za basi la ruti namba namba 375 , bado ni fumbo ambalo halijatatuliwa.

Comments