SAMIA FASHION FESTVAL 2 KUFANYIKA JUMAMOSI HII VISIWANI ZANZIBAR.
NA MWANDISHI WETU.
Tamasha la Samia Fashion Festival litatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii hapa nchini na linatarajiwa kuwakutanisha maelfu ya watanzania
Mwandaaji mkuu wa tamasha hilo ambaye pia ni mwanamitindo maarufu Khadija Mwanamboka amesema onyesho hilo litafanyika katika hoteli ya Golden Tulip,Zanzibar Jumamosi hii Novemba 30,2024
Amesema jaji mkuu katika tamasha hilo ni mwanamitindo wa Tanzania anayefanya shughuli zake nchini Marekani,Millen Maggese.
Mwanamboka amewataja majaji Wengine kuwa ni pamoja na ni Idriss Sultan ambaye ni muigizaji na mchekeshaji maarufu
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kama jaji mkuu wa tamasha hilo,Millen Magesse amesema kuwa uwepo wa tamasha hilo ni dhihirisho kuwa mitindo imekuwa kama alama ya utambulisho,urithi na fahari na pia litaonesha heshima ya jamii ya Tanzania kupitia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
"nilipopata habari za tamasha hili niliamua kuchukua ndege haraka kuja Tanzania na pia nakumbuka wakati napitia changamoto za kiafya Rais Dkt Samia wakati huo alinishika mkono na kunifuta machozi"amesema Millen.
Amesema tamasha hilo ni sehemu ya heshima kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na litahudhuriwa pia na watu mbalimbali maarufu hapa nchini akiwemo katibu Mkuu wa UVCCM,Jokate Mwegelo,Nancy Sumary, na wengineo huku akiwataka watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia.
Comments