MAENEO YA UWEKEZAJI KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI WILAYANI MAGU
MAENEO YA UWEKEZAJI KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI WILAYANI MAGU
Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari leo ijumaa Novemba 22, 2024 ameongoza kikao cha kawaida cha baraza la biashara la Wilaya .
Akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika ofisini kwake DC Nassari ameutaka uongozi wa Halmashauri kushirikiana na wananchi kwaajili ya kupata maeneno ya uwekezaji.
Aidha amesisitiza ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na wawekezaji ili kuinua na kukuza fursa za uchumi zinazopatikana Wilayani Magu kukuza uchumi wa Wilaya na taifa kwa ujumla.
Aidha ameitaka idara ya ardhi kuratibu mpango wa upimaji ardhi shirikishi ili kutenga maeneo ya uwekezaji ili yaweze kupata wawekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda na kilimo.
Comments