RC CHALAMILA AWAITA WANANCHI WA DAR ES SALAAM KUJITOKEZA KUPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
RC CHALAMILA AWAITA WANANCHI WA DAR ES SALAAM KUJITOKEZA KUPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwahimiza Wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kupiga kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024.
NA MWANDISHI WETU.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 nchini.
RC Chalamila ametoa wito huo leo Novemba 25, 2024 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema siku hiyo zoezi la upigaji kura litaanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
“Niwaombe wakazi wa Dar es Salaam kuzingatia taratibu na miongozo ya uchaguzi Ili watimize haki yao ya Msingi ya kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka, mtu yeyote akifika saa kumi hata ruhusiwa kupiga kura bali tu wale ambao wapo kwenye mstari kituoni” amesema RC Chalamila
Amesema Novemba 27, 2024 kila Mtanzania aliyetimiza Miaka 18 atashiriki Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji kwa kuchagua wenyeviti na wajumbe wake ambapo mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya mitaa 564.
Aidha amesema kuwa kwa mujibu wa Sensa iliyopita mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya watu zaidi ya Milioni 5 na laki tatu kwa mantiki hiyo watu waliofika miaka18 ni mil 3 kwa hiyo kwa mitaa yote inatarajiwa kuwa na wenyeviti na wajumbe.
Rc Chalamila ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha watu kujitokeza kwenda kupiga Kura ambapo amewasisitiza wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga Kura na kuchagua viongozi wanaowafaa.
Hata hivyo Rc Chalamila amesema kuwa mara nyingi kumekuwa na malalamiko machache kwamba mchakato wa Uchaguzi imekua na taarifa zilizofichama na kusababisha baadhi ya wenzetu kushindwa kupata na kujiandaa na Uchaguzi.
“Naamini wale wapenzi wa vyama vingi watajitokeza kupiga kura na kudumisha demokrasia iliyopo na kuchagua viongozi bora ili kujiletea maendeleo," amesema Rc Chalamila.
Ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anahimiza matumizi ya 4R lazima tujenge siasa njema,siasa ambazo tunakaa pamoja na kuziepuka zile siasa za chuki,
Rc Chalamila ametoa rai kwa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa ambapo itakuwa ni salamu kwa mataifa mengine Duniani kwamba Tanzania imeshavuka kihunzi cha demokrasia kwamba kila aliejiandikisha anapiga kura.
Rc Chalamila amesema inajulikana kuwa na Uchaguzi sio kigezo cha kuwa na demokrasia bali Uchaguzi unatakiwa kuwa wa wazi na kwa mantiki mhe Rais Samia Suluhu Hassan anataka Uchaguzi uwe huru na haki na ambao unaoakisi zile 4R alizoziasisi.
Sanjari na hayo Rc Chalamila amesema siku za kujiandikisha zilikuwa nyingi ila siku ya kupiga kura ni moja,hapa unaweza ukajiuliza kama una vituo vya kujiandikisha 1800 na wananchi wakatumia siku 5,6 mpaka 7 ila itumike siku 1 kupiga kwa idadi hiyohiyo Waliojiandikisha,
Amebainisha kuwa Vituo vya kupiga kura mkoani Dar es Salaam vimeongezaa ili kuhakikisha kila mtu anatimiza haki yake ya kuchagua Kiongozi anayemtaka na amewahakikishia usalama siku hiyo Wananchi wa Mkoa huo.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments