UKINUNUA KADI JANJA KWA 5000 MWENDOKASI DAR,UNAWEKEWA 3000 KAMA NAULI,DART YASEMA NI OFFER KWA AJILI YA SIKUKUU
KATIKA kuhakikisha wanawajali watumiaji wa Mabasi yaendayo kwa haraka (mwendokasi),Wakala wa mabasi yaendayo kwa haraka (DART), umewatangazia ofa watumiaji wake kuwa ukinunua kadi janja ya Sh.5000 itakupa ofa shiling 3000 kwa matumizi ya nauli.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt Athuman Kihamia, amesema ofa hiyo ni katika kuhimiza matumizi ya kadi janja kwa Abiria wanaotumia mabasi hayo.
Dkt Kihamia,amesema kumiliki kadi janja hizo Abiri anaweza kuchanja kwenye mageti yaliyo njia kuu na ndani ya mabasi.
“Ofa hii ni ya kipindi cha sikuku za mwisho mwaka, nawaomba watanzania kuchangamkia ofa hii nono wanapojiandaa kwa sikukuu za mwisho wa mwaka kwani zipo kadi chache kwenye ofa hii “Amesema Dkt Kihamia.
Comments