Wadau wapongeza sera ya kuwawezesha wazawa kiuchumi.

 WADAU WAPONGEZA SERA YA KUAWEZESHA WAZAWA KIUCHUMI.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam.

Serikali imesema kuwa mchakato wa kutengeneza rasimu ya Sera ya kuwawezesha wazawa (Local Content) kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia sekta mbalimbali mtambuka utasaidia  kujenga uchumi wa nchi pindi utakapokamilika.

Akizungumza wakati wa Kikao cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara cha Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam,  Katibu Mkuu, wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonaz amesema kuwa ili kuleta utekelezaji jumuishi kwa sekta zote za umma na binafsi, kuna umuhimu wa kutungwa kwa sera ya kitaifa ili kutoa fursa zaidi kwa Watanzania kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi.

“Malengo ya sera hii, pamoja na mambo mengine, kuimarisha ushiriki wa Watanzania na taasisi za Kitanzania kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi kama inavyopendekezwa na wadau” amesema Dkt Yonaz, ambaye ndiye Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho.

Amesema kuwa kupitia sera hiyo, Serikali inakusudia kufanya maboresho ya kuimarisha mifumo na sheria, ili Watanzania wawe na mazingira wezeshi ya ushindani katika soko la biashara.

Aidha, alisema kuwa lengo la utungaji wa sera hiyo ni kuwezesha mifumo mbalimbali ya utendaji Serikalini kusomana kwa njia ya kidijitali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).

“Tanzania inaenda kuwa na mazingira bora ya ufanyaji kupitia ujio wa sera hii  ya taifa,” alisema.

Mapendekezo hayo ya kamati ni  sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mwenyekiti wa TNBC, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Juni mwaka huu .

Comments