DC KINONDONI AWAPA 5 MAFIA BOXING PROMOTIONS KWA KUJA NA KNOCK OUT YA MAMA,AWAITA 'WANADARISALAMA'



NA MWANDISHI WETU 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Saad Mtambule amepongeza kampuni ya mchezo wa ngumi hapa nchini Mafia Boxing Promotions kwa kuandaa pambano maalum kwa ajili ya kuenzi Kazi  zinazofanywa na Serikali litakalofanyika jijini Dar Es Salaam.


Pambano hilo ambalo litawakutanisha mabondia kutoka ndani na nje ya nchi litafanyika Disemba 26 mwaka huu ambayo itakuwa ni siku ya pili ya sikukuu ya Christmas yaan boxing day.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa Habari uliofanyika katika ofisi za Mafia boxing Promotions zilizopo Magomeni Usalama Jijini Dar Es Salaam Mtambule alisema kuwa katika pambano hilo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Kasim Majaliwa (Mb)anatarajiwa kuwa ndiye Mgeni rasmi.

Mtambule alisema  mchezo wa ngumi umekuwa na hamasa kubwa kwa siku za hivi karibuni na kampuni ya Mafia boxing imeonyesha kwa vitendo kuunga mkono juhudi za Serikali katika michezo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafia boxing Promotions Ally Zayumba amemshukuru Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwapa ushirikiano katika maandalizi yote ya pambano la  knock out ya mama sehemu ya pili.

Amesema pambano hilo ambalo litapigwa Siku ya boxing day Disemba 26,2024 ni ili kuonyesha kuwa wanaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya michezo hapa nchini.

Alisema zaidi ya wageni 40 kutoka nie ya nchi wakiwemo mabondia ambao wataanza kupokelewa kuanzia leo jumatatu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)Jijini Dar Es Salaam.

Aliongeza kuwa mikanda mitano ya ubingwa itakagombewa kwa wakati mmoja jambo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ni pamoja na  WBO,IBA,WBA,BST ambapo mabondia mbalimbali wa Tanzania watapambana na mabondia kutoka nje ya nchi.

"nawakaribisha watu wote pale SuperDome,Masaki kuanzia saa 7 mchana  siku ya pambano kwani tutaanza mapema na kumaliza mapambano yote kabla ya saa 6 usiku na pia niwaalike siku ya Christmas ambapo mabondia wote watapima uzito pale Coco beach"alisema Zayumba 

Naye msemaji wa kampuni ya Mafia boxing Promotions ambaye pia ni mwigizaji J Mafufu alisema kuwa hakuna mkanda hata mmoja ambao utaachwa na mabondia wa Tanzania na baadaye mikanda hiyo itapelekwa Ikulu kutokana na mapambano hayo kuwa maalum kwa ajili ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,hivyo amewasihi watanzania wajotokeze kwa wingi siku hiyo.

Comments